
Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
Dar es Salaam. Baraza la Wazee wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) limempongeza Mzee Kingunge Ngombale Mwiru kwa kuachana na Chama cha Mapinduzi (CCM) na kujiunga na upande wa mabadiliko kikisema ni jambo la kuigwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Katibu wa Baraza hilo, Rodrick Lutembeka alisema Mzee Kingunge amefanya uamuzi mgumu na wenye busara japokuwa umekuwa ni pigo kwa CCM.
“Tunampongeza kwa sababu alizozitoa ambazo ni kukosekana kwa demokrasia ndani ya chama,” alisema Lutembeka na kuongeza kwamba Watanzania wanahitaji mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na hawawezi kuyapata ndani ya CCM kwani viongozi wake hawako tayari kuwaletea.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Chadema, Arcado Ntagazwa alisema kanuni ya sayansi ya siasa inasema chama chochote cha siasa kinazaliwa, kinakua na baadaye kinakufa, hivyo wakati wa CCM kufa umefika.
No comments :
Post a Comment