dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

Dk. Sinare atangaza kujing'atua CCM.

Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Eve Hawa Sinare, ametangaza kujivua uanachama wa chama hicho.
Dk. Sinare amesema amefikia uamuzi huo kutokana na CCM kushindwa kutatua matatizo ya vijana na umaskini kwa kutoa huduma bora ya afya, elimu, maji na umeme hata wakishinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
 
Dk. Sinare alitangaza hayo juzi jijini Dar es Salaam, mbele ya waandishi wa habari.
 
“Kuanzia leo (juzi, nimejitoa CCM,” akisisitiza huku akisema licha ya kujitoa katika chama hicho tawala, bado hajaamua kujiunga na chama kingine chochote cha siasa.
 
Hata hivyo, Dk. Sinare alisema anaunga mkono mabadiliko ya kweli ndani ya nchi.
 
Uamuzi wa Dk. Sinare kujitoa CCM unakuja siku chache baada ya aliyekuwa kada wa chama hicho, Balozi Juma Mwapachu, kutangaza kujiengua katika chama hicho na akitanguliwa na mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale-Mwiru aliyetangaza kujitoa CCM, Oktoba 4, mwaka huu.Dk. Sinare ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kahawa, Mwenyekiti wa kuchunguza matatizo ya vyuo vikuu na Mjumbe wa Bodi ya Mashirika ya Umma ambaye hivi sasa ni Wakili wa kujitegemea, alisema kwa miaka 53 madarakani, elimu nchini ni duni huku viongozi wakichukulia uongozi ni ajira ya kujitajirisha kuliko kuangalia matatizo ya Watanzania.
 
Alisema kuwa hivi sasa vijana wengi hawana ajira zenye tija wakati viongozi wanajilimbikizia mali na kujilipa mamilioni ya fedha kwenda kuhonga na kununua kura kila inapofika kipindi cha uchaguzi.
 
Dk. Sinare alisema Serikali ya CCM imewakosea wananchi, kwani kwa miaka yote ilipokuwa madarakani, huduma za afya zimekuwa duni huku viongozi bila woga wakisafiri kwenda nje ya nchi kupatiwa matibabu ya gharama kubwa na hospitali zikikosa dawa.
 
Alisema huo ni mfumo mbaya uliowekwa na CCM kuwanufaisha viongozi huku wananchi wakiteseka kwa kukosa huduma bora na uongozi kutoka kwao.
 
Aliongeza kuwa vyombo vya usalama, Polisi na muundo mzima wa serikali pamoja na mashirika ya umma, yamekuwa yakitumika kukampenia chama tawala.
 
Aidha, alisema chini ya uongozi wa CCM, kila Mbunge hulipwa mafao makubwa na yasiyo na ulazima pindi Bunge linapovunjwa.
 
Alisisitiza kuwa mambo yote mabaya yaliyofanywa na CCM na kuifanya nchi kuwa katika hali mbaya, yanahitajika mabadiliko ili kuokoa ufujaji wa fedha za umma ziende kuwahudumia Watanzania.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment