dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

Jenerali Mwamunyange sasa aibukia Ngerengere.

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davis Mwamunyange, (pichani) ameibukia katika Kamandi ya Anga Kizuka iliyopo Ngerengere, mkoani Morogoro wakati Rais Jakaya Kikwete, akizindua uwanja wa Ndege wa Kamandi hiyo.
 
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Rais Kikwete alisema kuwa katika miaka 10 ya uongozi wake, amefanya mambo mengi kwa Watanzania pamoja na kuliacha Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) likiwa katika hali nzuri ya kiutendaji.
 Alisema hakuna nchi inayoweza kupata maendeleo mbalimbali kama haina jeshi imara kutokana na kuwapo vitendea kazi vya kutosha na madhubuti vinavyoimarisha jeshi hilo.
 
 “Nalishukuru Jeshi la Serikali ya China kwa kutujengea uwanja huo wa kisasa wenye urefu wa mita 3,000 ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa shughuli zote za Kamandi ya Anga hapa nchini kwetu…Serikali ya China imekuwa rafiki wa kweli wa Tanzania kwa muda mrefu ikiwamo kutusaidia kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo,” alisema Rais Kikwete. Aidha, alisema serikali ya awamu ya tano haina budi kuhakikisha inaendeleza mahusiano hayo kwa faida ya watu wa nchi hizo mbili.
 
Kwa upande wake, Jenerali Mwamunyange alisema katika kipindi chote cha uongozi wa Rais Kikwete, ameimarisha JWTZ na kutimiza mahitaji ya jeshi hilo.
 
Alisema pamoja na changamoto ndogo zilizobaki, lakini anaamini serikali ijayo itazifanyia kazi na kuendeleza pale alipoishia ili kuwa na jeshi imara.
 
 Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk. Hussein Mwinyi, alisema uwanja huo utaliwezesha JWTZ kufanya mazoezi yake na kuwasaidia wananchi wanaotumia usafiri wa ndege kutoka mkoa huo kwenda sehemu mbalimbali.
 
Aliipongeza Serikali ya China kwa kuisaidia Tanzania kwa mambo mbalimbali ya kimaendeleo na kuifanya kuwa moja ya nchi zinazoendelea kukua kwa haraka.
 
Hivi karibuni mitandao ya jamii iliripoti kuwa Jenerali Mwamunyange amelishwa sumu, lakini serikali ilizikanusha.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment