dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Kikwete awahakikisha waangalizi kimataifa amani, utulivu!


Rais wa Tanzania, Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
By Tumaini Msowoya, Mwananchi
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amewahakikishia viongozi wa waangalizi wa kimataifa kuwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu utafanyika kwa amani na utulivu ikilinganishwa na zilizopita.
Rais Kikwete alitoa kauli hiyo jana, wakati akizungumza na viongozi hao Ikulu walikokwenda kujitambulisha.
Viongozi hao ni Rais mstaafu wa Nigeria, Goodluck Jonathan anayeongoza ujumbe wa waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola na Rais mstaafu wa Msumbiji, Armando Emilio Guebuza wa ujumbe wa Umoja wa Afrika (AU).
“Uchaguzi wa mwaka huu utakuwa wa amani na utulivu kuliko miaka yote, kampeni zimeendeshwa kwa amani na utulivu. Nina imani kubwa kabisa kuwa utakuwa huru na wa amani zaidi,” alisema
Jonathan alisema ujumbe wake una wataalamu waliobobea kwenye siasa, uchaguzi, waandishi wa habari na vijana na una jukumu la kufuatilia uchaguzi huo kabla, wakati na baada ya kupiga kesho.
Waangalizi kutoka Jumuiya ya Madola wametoka Afrika Kusini, Botswana , India, Jamaica, Kenya, Malaysia na New Zealand.
Wengine wanatoka Papua New Guinea, Singapore, Sri Lanka, Trinidad na Tobago, Uganda na Uingereza. Waangalizi kutoka AU wametoka Afrika Kusini, Burundi, Botswana, Cameroon, Chad, Ethiopia, Gambia, Ghana, Kenya, Lesotho, Malawi, Msumbiji, Nigeria, Somalia, Sierra Leone, Swaziland, Uganda, Shelisheli na Zambia. Waangalizi hao watasaidiwa na Kamisheni ya Afrika, Bunge la Afrika na Taasisi ya Uchaguzi na Demokrasia ya Afrika katika kazi yao hiyo.
Rais awaonya watumishi wa umma
Katika tukio jingine; Rais Kikwete amesema itakuwa vigumu Tanzania kupiga hatua ya maendeleo ikiwa watumishi wa umma wataendeleza ukiritimba kwenye sekta hiyo. Akizungumza juzi wakati na watumishi wa umma katika hafla ya kumuaga, Rais aliyataja maeneo yanayotakiwa kubadilisha mfumo katika kufanya uamuzi kuwa ni Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Sekta Binafsi na Sekta ya Umma (PPP), viongozi wa wizara na sekta ya sheria.
Alisema kuna wawekezaji ambao walitaka kuwekeza nchini lakini kutokana na ukiritimba wamelazimika kwenda nchi nyingine.
“Tangu naingia madarakani miaka 10 iliyopita, nasikia uwekezaji kwenye shamba la mifugo la Ruvu, mpaka naondoka uamuzi haujafanyika wakati kampuni iliyotaka kuwekeza imeanza kazi Nigeria na Gabone, sisi hatujafikia uamuzi,” alisema.

No comments :

Post a Comment