dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Balozi Karume awavaa wanaotaka mamlaka kamili Zanzibar.

  �Adai wamekuwa wakikipotosha kizazi cha sasa kwa kueleza uongo, huku wakitumia uhuru wa kujieleza na demokrasia kutekeleza malengo yaliyojificha

Balozi Mstaafu, Ali Abeid Karume.
Balozi Mstaafu, Ali Abeid Karume, amesema baadhi ya wanasiasa  wanaojinadi kupigania maslahi ya Zanzibar na kutaka ipate mamlaka kamili wana lengo la kuvunja Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwa kisingizio cha demokrasia na uhuru wa kutoa maoni.  
 
Amesema wanasiasa hao wamekuwa wakikipotosha kizazi cha sasa kwa kueleza uongo, huku wakitumia uhuru wa kujieleza na demokrasia ya vyama vingi kutekeleza malengo yao yaliyojificha.
 
Balozi Karume alisemama hayo kwenye kongamano la amani lililoitishwa na Jumuia ya House of Inspiration ya visiwani  Zanzibar, mjini hapa juzi. 
 
Alisema Zanzibar ilipata mamlaka yake  kamili na kuwa huru kuanza Januari 12, 1964 baada ya visiwa hivyo kutawaliwa na Sultan wa kigeni kwa miaka 160 tangu mwaka 1804 hadi1964 yalipofanyika mapinduzi matukufu.
 
Alisema wakati mataifa mawili ya Zanzibar na Tanganyika yakiungana Aprili 26, 1964, kila upande ulikuwa huru, ukiwa na madaraka kamili uamuzi wa kuungana ulipofikiwa kulikuwa na makubaliano ya pande hizo mbili ambayo yanatambuliwa na Umoja wa Mataifa.Balozi Karume ambaye ni mtoto wa pili wa Rais  wa Kwanza  wa Zanzibar, Hayati Abeid Amani Karume, alisema aina ya muungamo wa nchi mbili za Tanganyika na Zanzibar uliozaa Tanzania hauna tofauti na wa Uingereza wenye nchi nne za England, Northern Island, Wales na Scotland, huku taifa hilo likiwa na kiti kimoja katika Umoja wa Mataifa, sarafu moja, benki kuu moja na wizara ya mambo ya nje moja.
 
"Ikiwa wanapitapita huku na huko ili kutaka kuvunja Muungano ni heri weseme na wala wasifiche, kabla ya mwaka 1964 Zanzibar haikuwa na mtu aliyejiita raia, wote walikuwa miliki ya Sultan, madaraka na mamlaka kamili ya Zanzibar  yalianza Januari 12, 1964," alisema.
 
Alisema si kweli kwamba kabla ya mapinduzi Zanzibar ilikuwa na hati ya kusafiria, sarafu yake na wizara ya ulinzi kama inavyodaiwa na baadhi ya wapinzani, bali masuala hayo yalikuwa chini ya ufalme wa kigeni uliolindwa na Uingereza huku ukijenga matabaka katika jamii.
 
Balozi Karume aliwahimiza wananchi na  washiriki wa kongamano hilo katika visiwa vya  Unguja na Pemba kuwa makini dhidi ya hadaa na hila za baadhi ya wanasiasa ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakifanya  juhudi kuwagawa wananchi wa Tanzania Bara na Zanzibar. 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment