dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

Kingunge ataka wazee wawaunge mkono vijana kuleta mabadiliko.

Mwanasiasa mkongwe na mwanamabadiliko, Kingunge Ngombale-Mwiru.
Mwanasiasa mkongwe na mwanamabadiliko, Kingunge Ngombale-Mwiru, amewataka wazee kuwaunga mkono vijana ili kuleta mabadiliko ya kiuongozi nchini na kukiondoa chama tawala madarakani.
 
Hata Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, wakati anatafuta uhuru wa nchi yetu, wazee ndiyo waliomtia nguvu hadi kusababisha kufanya mabadiliko ya kutoka kutawaliwa hadi kutawala nawaomba wazee wenzangu kuungana na vijana kufanya mabadiliko, alisema.
 
Akizungumza na Nipashe kwa  njia ya simu jana, alisema ni wakati wa vijana kufanya mabadiliko ya kiuongozi, lakini kubwa ni wazee kuwaunga mkono. Alisema wapo viongozi waliopo madarakani wanao amini nchi ni mali yao na wengine hawatakiwi kufanya lolote, lakini wanajidanganya kwani bila vijana hakuwezi kuwa na mabadiliko ambayo yataungwa mkono na vijana.
 
Naye mjumbe mstaafu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (CCM), Hussein Mashimba, alisema ni wakati wa wazee kuungana na vijana kufanya mabadiliko ya uongozi.
 
Mashimba alisema kuweza kufanya mabadiliko pekee bila wazee kuwaunga mkono vijana, hakutoshi kuleta mabadiliko ya kweli, hivyo ni lazima wazee kushikamana na kufanya maamuzi sahihi. Alisema uungaji mkono wa wazee kwa vijana, unatakiwa kufanyika Jumapili (kesho) wakati nchi itakuwa inafanya Uchaguzi Mkuu wa Rais, wabunge na madiwani.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment