dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

MASHEIKH WAMTAKA LOWASSA!

Mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa.
Kamati  ya Masheikh na Maimamu wa Mkoa wa Dar es Salaam, imewataka Waislamu kote nchini, kushiriki katika kupiga kura kwa amani na kuhakikisha wanaleta mabadiliko kwa kumpigia kura mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa, pamoja na wagombea wote wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa kamati hiyo, Sheikh Said Omar Rico, alisema fikra mgando zinahitaji kuondolewa, kwani kwa muda mrefu Chama tawala ambacho ni Chama cha Mapinduzi (CCM), kimeshindwa kufanya mabadiliko ya kweli kwa Watanzania.
Alisema anawaonya masheikh ambao wanatumika kisiasa kwa kuwatisha Waislam na kuwaambia wasimchague mgombea huyo, kwa madai ya kuwa ni mdini halina ukweli.
Alisema Oktoba 17, mwaka huu mashekh wa mkoani Mwanza katika sherehe za kuadhimisha mwaka mpya wa kiislam, zilitolewa tuhuma na kumshambulia Lowassa, kwamba ni mdini kwa kuwa ni rafiki wa karibu wa Askofu Josephat Gwajima.
Alisema mashekh hao, walipaswa kuzungumzia hali ya waislam na uislam kwa kipindi cha mwaka uliopita mahali walikotoka, walipo na waendako, badala yake waliamua kufanya kazi ya kumshambulia mgombea huyo anayewakilisha Ukawa.
UKAWA:  TUMEJIPANGA
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),  umesema umejiandaa  kuongoza nchi  na kwamba tayari timu ya wataalam kutoka ndani ya vyama hivyo, inafanya kazi ya kupanga mikakati ya kuhakikisha mambo muhimu na ya msingi yanashugulikiwa ndani ya siku 100 za mwanzo baada ya kuingia Ikulu.
Kadhalika, umesema unatarajia kuingia madarakani kwa njia halali na kukishauri Chama Cha Mapinduzi (CCM), kutotafuta kubakia madarakani kwa njia zisizo halali.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof. Mwesiga Baregu, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam. Alisema Ukawa ina timu nzuri ya kuishauri serikali yao, na itakuwa ndogo itakayobeba wizara za msingi tu.
Pia alisema tayari wanawasiliana na Umoja wa Mataifa, ili kuhakikisha unafuatilia kwa makini uchaguzi huo ili kuhakikisha unafanyika kwa uhuru, uwazi, uhuru na kwa haki.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment