dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 23, 2015

Lowassa na kaulimbiu ya mabadiliko

Mgombea wa urais kwa tiketi ya Chadema anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa akihutubia katika moja ya mikutano ya kampeni ya chama hicho. 
By Fidelis Butahe, Mwananchi
Ilikuwa miaka, mwaka, miezi na sasa zimesalia siku chache kabla ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema na Ukawa, Edward Lowassa kujua hatima ya “Safari ya Matumaini” aliyoianza takriban miaka 20 iliyopita.
Baada ya kuenguliwa mwaka 1995 na kujizuia kuingia kwenye mbio za kuelekea Ikulu mwaka 2005, Lowassa alipata kikwazo cha kuendelea na safari yake mwaka huu wakati Kamati Kuu ya CCM ilipoengua jina lake, lakini aliamua kuendelea nayo akisema “CCM si mama yangu” na kujiunga na Chadema iliyompa fursa ya kugombea urais.
Lowassa, Waziri Mkuu wa kwanza kuhama chama tawala, aliondoka CCM akipinga kukiukwa kwa katiba ya chama hicho katika kumpata mgombea urais.
Lakini alikuwa mjanja hata kabla ya kuhama CCM. Wakati akisaka wanachama wa CCM wamdhamini kugombea urais, alizunguka nchi nzima, akifanya mikutano mikubwa ya hadhara na kusisitiza wananchi wajiandikishe kupiga kura. Wagombea wenzake hawakuzunguka mikoa mingi.
Ni kwa jinsi hiyo, alikuwa ameshajijengea wigo mkubwa wa mashabiki, ambao si ajabu kuwa ndio unaomfuata leo kwenye mikutano yake mingi, ukiunganishwa na ule uliojengwa kwa muda mrefu na Chadema.
Staili mpya ya kampeni
Baada ya kuwekewa mizengwe kwa kunyimwa Uwanja wa Taifa kuzindulia kampeni zake na baadaye kuwapo kizaazaa katika kutumia viwanja vya Jangwani, Lowassa na Ukawa walianza kampeni Agosti 29, lakini kabla ya hapo alitetemesha jiji.
Agosti 25 alisafiri kwa daladala kuangalia hali ya usafiri wa umma katika Jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni siku ya tatu tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mkuu.
Alifika kituo cha daladala cha Gongo la Mboto, saa 1:51 asubuhi akiwa katika msafara wa magari matano.
Siku iliyofuata, Lowassa alitembelea masoko ya Tandale na Tandika kwa lengo la kukutana na makundi ya watu wenye kipato cha hali ya chini, kujua matatizo yanayowakabili ili aweze kuwasaidia akiwa rais.
Msafara wake kwenda katika Soko la Kariakoo ulizuiwa na polisi ambao siku hiyo walitoa tamko la kupiga marufuku ziara za mgombea huyo kwa madai ya usalama wake na kudhibiti uwezekano wa kuibuka vurugu na kuvunjika kwa amani.
Lakini Lowassa alibadili staili yake ya kampeni na kuanza kukutana na makundi mbalimbali katika mpaka Agosti 29 alipoungana na viongozi wa Ukawa kuzindua kampeni kwenye viwanja vya Jangwani ambavyo vilifurika maelfu ya wananchi.
Siku hiyo, umati wa watu uliofurika kwenye viwanja hivyo ulimshuhudia Lowassa akihutubia kwa dakika zisizopungua dakika 12,  akitangaza vipaumbele vya Chadema kuwa ni “elimu, elimu, elimu” na kuomba kura kwa mashabiki.
Kuhutubia kwa dakika chache ndio imekuwa tabia yake kwenye mikutano yote na ni mara chache hufikia dakika 18.
Ushangiliaji 
Kabla ya uzinduzi wa kampeni hizo, mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alianzisha staili ya kumshangilia mgombea urais huyo, akisema hutumiwa kote duniani.
Alisema wananchi na wafuasi wa Chadema wanatakiwa kuzungusha mikono yao hewani, linapotamkwa jina la la Lowassa akiwataka wajibu, “mabadiliko”, na linapotamkwa neno “mabadiliko” nao waitikie, “Lowassa”.
Kuzungusha mikono hewani ni ishara inayotumiwa kumaanisha mabadiliko, hasa kwenye mchezo wa mpira wa miguu wakati mwamuzi anapotaarifiwa kuwa kuna timu inataka kubadili mchezaji.
Staili hiyo imekubalika kwa wengi, kufikia hatua ya wananchi kuitumia kushangilia katika kumbi mbalimbali za burudani na hata kwa mashabiki wa soka.
Staili hiyo sasa ni kama salamu kwani ni jambo la kawaida kuwaona wafuasi na wanachama wa Chadema kila sehemu.
Unayajua mahaba ya Lowassa?
Ukifuatilia mikutano ya kampeni ya Lowassa lazima utasikia akitamka neno “mahaba”, unajua kwanini analitamka?
Kabla ya kuzungumza jambo lolote Lowassa huanza kutamka maneno haya, “Kuna rafiki yangu mmoja wa Zanzibar aliwahi kuniambia kuwa haya si mapenzi, haya ni mahaba”.
Sijui rafiki huyu ni yupi, lakini Lowassa hutumia maneno haya kutokana na mikutano yake ya kampeni kuhudhuriwa na maelfu ya wananchi, hivyo huamini kuwa wingi huo wa watu unatokana na mapenzi waliyonayo kwake.
Lowassa na dhana ya mabadiliko
Pamoja na kurushiwa shutuma za kila aina kutoka kwa wapinzani wake wanaomhusisha zaidi na kashfa ya Richmond, Lowassa ameendelea kuonekana nembo ya mabadiliko kwa Watanzania hasa wanaounga mkono vyama vya upinzani.
Amekuwa akiahidi mabadiliko, akisema wananchi hawajanufaika na uhuru kwa zaidi ya miaka 50. Anasema anachukia umaskini, anaahidi elimu bure, kuboresha mazingira bora kwa waendesha bodaboda, mama lishe na wafanyabiashara wadogo, kuondoa tatizo kubwa la maji, kuunda tume za kuchunguza mikataba ya madini na migogoro ya wakulima na wafugaji.
Anasema Serikali yake itaendeshwa kwa mchakamchaka na kwamba mabadiliko atakayoyaleta yataonekana hata kwa mamalishe na madereva bodaboda, ambao mara kadhaa amekuwa akiwataja kuwa rafiki zake.
Bila ya shaka, kampeni hizo zitamfanya mwaka huu awe na matarajio makubwa zaidi kwenye safari yake ya matumaini.

No comments :

Post a Comment