Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 28, 2015

Ni mtifuano Magufuli, Lowassa.

Wagombea wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa na wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli.
Wakati leo ni siku ya tatu tangu kuanza kutangazwa kwa matokeo ya urais kutoka kwenye majimbo mbalimbali nchini, mchuano ni mkali kati ya mgombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli na wa Chadema, Edward Lowassa.
 
Tofauti na matarajio ya Watanzania wengi kuwa matokeo yatatangazwa ndani ya siku nne, leo ni siku ya tatu hadi saa 10 jioni na majimbo yaliyotangazwa ni 88 kati ya 264 yaliyofanya uchaguzi Oktoba 25, mwaka huu.
 
Kwa mujibu wa matokeo yaliyotangazwa kwa nyakati tofauti juzi na jana na Tume ya Taifa ya Uchaguzi ( Nec), hadi saa 10 jioni katika majimbo 88 yanaonyesha kuwa Dk. Magufuli anaongoza kwa kura 1, 693, 895  akifuatiwa na Lowassa mwenye kura 1,242,976.
 
Matokeo hayo yanaonyesha kuwa Dk. Magufuli anaongoza katika majimbo 65 huku Lowassa akiongoza katika majimbo 23, akiachwa kwa kura 450,919.
 
Idadi za kura kwa kila jimbo ni kama ifuatavyo; Katika jimbo la Chalinze CCM kura 52,212, Chadema 21,380; Jimbo la Chonga CCM 1,740, Chadema 3,860; Jimbo la Chumbuni CCM 5,096 Chadema 4,450; Jimbo la Ileje CCM 26,368,  Chadema 15,651; Jimbo la Kojani CCM 2,703, Chadema 3,351; Jimbo la Kilindi CCM  33,941, Chadema 12,123.Jimbo la Korogwe Mjini CCM 17,168 Chadema 9,034; Jimbo la Kohani CCM 6,245, Chadema 2,684; Jimbo la Lupembe CCM 23,061, Chadema 7,466;Jimbo la Mdaba CCM 13,949, Chadema 4,735; Jimbo la Masasi CCM  24,637,  Chadema 16,778; Jimbo la Mbeya Vijijini CCM 62, 662, Chadema 47,038; Jimbo la Mkwajuni CCM 4,686, Chadema 3,314, Jimbo la Momba CCM 28,978 , Chadema 24, 418.
 
Mengine ni Jimbo la Monduli Chadema 49,675 , CCM 11,355; Jimbo la Mpendae CCM 4,192, Chadema 4,048; Jimbo la Mwanga CCM 25, 738, Chadema 15, 148; Jimbo la Namtumbo CCM 44,061, Chadema 23,039; Jimbo la Newala Mjini CCM 21,269,  Chadema 16,980; Jimbo la Newala Vijijini CCM 29,799,  Chadema 13,388.
 
Jimbo la Muhambwe CCM 37,746, Chadema 22,804; Jimbo la Jang’ombe
CCM 6,577, Chadema 2,839; Jimbo la Jang’ombe CCM 6,577, Chadema 2,839; Jimbo la Malindi CCM 2,581, Chadema 5,622; Jimbo la Tabora Kaskazini CCM  38,050, Chadema 12,410; Jimbo la Unguja Kaskazini CCM 5,592, Chadema 1,019.
 
Jimbo la Ole CCM 618 Chadema 5,251; Jimbo la Ziwani CCM 592, Chadema 6,067; Jimbo la Wawi CCM 1,748, Chadema 5,216; Jimbo la Ulanga CCM 32,297, Chadema 20,489; Jimbo la Igalula CCM 28,747, Chadema 8,593; Jimbo Tumbatu, CCM 5,720, Chadema 3,967; Jimbo la Tandahimba, Mtwara CCM 49,098, Chadema 46,288, Jimbo la Solwa, Shinyanga CCM 66,096, Chadema 23,510.
 
Mengine ni Jimbo la Siha, Kilimanjaro CCM 18,252 Chadema 22,572; Jimbo la Ruangwa CCM 34,516, Chadema 26,827; Jimbo la Newala Mjini CCM 21,269, Chadema 16,980; Jimbo la Newala Vijijini CCM 29,799, Chadema 13,958; Jimbo la Njombe Mjini CCM 33,626, Chadem 20, 368; Jimbo la Singida Mjini CCM 36,035, Chadema 19,007; Jimbo la Lindi Mjini CCM 21,088, Chadema 17, 607, 03.
 
Jimbo la Kojani CCM 1,561, Chadema 9,982; Jimbo la Wete CCM 958, Chadema 5,119; Jimbo la Gando CCM 881, Chadema 5,903; Jimbo la Mtambwe CCM 428, Chadema 6,937; Jimbo la Mgogoni CCM 710, Chadema 6,506.
 
Jimbo la Kisarawe CCM 24,086, Chadema 13,093; Jimbo la Mbinga Mjini
CCM 29,295, Chadema 11,695; Jimbo la Nanyamba CCM 24,904, Chadema 16,992; Jimbo la Moshi Mjini CCM 28,909, Chadema 49, 379; Jimbo la Mkinga CCM 23,798, Chadema 15,142; Jimbo la Peramiho CCM 32,505 , Chadema 11,291;
 
Jimbo la Shaurimoyo CCM 5,849, Chadema 113; Jimbo la Fuoni CCM 956, Chadema 420; Jimbo la Kikwajuni CCM 6,317, Chadema 3,669; Jimbo la Mpanda Mjini CCM 37,321, Chadema 12,791; Jimbo la Mchinga CCM 13,948, Chadema 12,936; Mwera CCM 6,430, Chadema 5,865; Jimbo la Ugwini CCM 2,303, Chadema 2,822; Jimbo la Uzini CCM 6,537, Chadema 1,864; Jimbo la Nkasi Kaskazini CCM 25,837, Chadema 19,891.
 
Mengine ni Chakechake CCM 1,253, Chadema 5,209; Nkasi Kusini CCM 21,572, Chadema 13,550; Jimbo la Nkenge CCM 42,568, Chadema 25,840; Jimbo la Amani CCM 4,322, Chadema 3,157; Jimbo Nungwi CCM 4,134, Chadema 4,853.
 
Jimbo la Chwaka CCM 6,537, Chadema 1,864; Jimbo la Mtama CCM 29,625, Chadema 20, 841; Jimbo la Tunguu CCM 8,519, Chadema 2,923; Jimbo la Biharamulo CCM 44,943, Chadema 28,576; Jimbo la Arush Mjini CCM 65,107, Chadema 150,786; Jimbo la Kibaha Vijijini CCM 20,505, Chadema 11,344; Jimbo la Mwanakwerekwe CCM 4,206, Chadema 4,406.
 
Mengine ni Jimbo la Nachingwea CCM 46,485, Chadema 30,252; Jimbo la Mafia CCM 11,155, Chadema 9,363; Jimbo la Mkuranga CCM 45,710, Chadema 36,478; Jimbo la Welezo CCM 2,615, Chadema 2,582; Jimbo la Magomeni CCM 5,716, Chadema 3,711.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment