dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, October 24, 2015

RC awaonya wagombea wanaokiuka sheria



Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Rufunga
By Stella Ibengwe, Mwananchi
Shinyanga. Uongozi wa Mkoa wa Shinyanga umewaonya baadhi ya wagombea wanaodaiwa kutembea na silaha za jadi kwenye magari yao kuwa watachukuliwa hatua kwa kukiuka sheria na taratibu za Uchaguzi Mkuu.
Onyo hilo lilitolewa juzi na Mkuu wa Mkoa huo, Ally Rufunga kwenye mkutano wa wadau mbalimbali mkoani hapa.
Rufunga alisema Serikali haipo tayari kushuhudia vurugu zikitokea kwa kuwa kila mwananchi ana haki ya kupiga kura bila kuvunja amani nchini.
“Hatuwezi kuvumilia mambo haya, unatengeneza kombeo kwa ajili ya kumuumiza mwenzako hivi unajisikiaje?” alihoji Rufunga.
“Kuna watu wanataka kutumia kigezo cha kulinda kura vituoni kwa lengo la kuwazuia wenzao wakiwamo wazee na wanawake kupiga kura, yote haya tumeyabaini. Kwanza inasikitisha kusikia baadhi ya watu wametengeneza kombeo kwa ajili ya kuumiza wenzao,” alisema.
Kwa upande mwingine, aliwataka viongozi wa siasa na wadau hao kuhamasisha jamii idumishe amani kwa sababu hilo ni jukumu la kila mmoja.
Mwakilishi wa Shirika la Save the Children, Herman Mbunda aliwataka wadau kuelimisha wananchi jinsi ya kulinda watoto huku akivitaka vyombo vya dola kuimarisha ulinzi na usalama kwa kundi hilo.
Katibu wa Dawati la Jinsia la Polisi Mkoa wa Shinyanga, Pili Misungwi, aliwaomba wananchi kuwapuuza watu wanaowalazimisha kujiunga kwenye makundi ya vurugu.

No comments :

Post a Comment