Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, October 9, 2015

Samia aombwa wodi ya watoto njiti!


Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Samia Suluhu akihutubia katika moja ya mikutano ya chama hicho. Picha na Maktaba
By Beatrice Moses, Mwananchi
Kwimba.  Wakazi wa wilaya ya Kwimba wamemuomba mgombea mwenza wa urais kupitia CCM, Samia Suluhu Hassani awajengee wodi ya watoto waliozaliwa kabla ya wakati (njiti) ili kuwanusuru uhai wao endapo chama chake kitashinda nafasi ya urais.
Ombi hilo limewasilishwa na mgombea ubunge wa jimbo la Kwimba, Mansoor Hiran leo kwenye mkutano wa kampeni wa Samia uliofanyika kwenye Kata ya Ngudu, wilayani hapa.
"Kuna changamoto kadhaa tumezitatua na nyingine tunaendelea kuzitafutia ufumbuzi lakini hili suala la ujenzi wa wodi ya watoto njiti utusaidie utakapoingia madarakani," amesema Hirani huku akishangiliwa na wakazi hao.
Akizungumzia hilo, Mganga Mkuu wa wilaya Kwimba, Paulo Swakala amesema kukosekana kwa wodi hiyo kumesababisha watoto hao kuhudumiwa katika mazingira yasiyo sahihi hivyo kusababisha wengine kupoteza uhai.
Akihutubia katika mkutano huo, Mama Samia aliahidi atakapoingia madarakani atabeba jukumu la kuhakikisha anashirikiana na viongozi wengine kukabiliana na changamoto zinazowakabili wajawazito.
"Tunafahamu vipo vifo vya mapenzi ya Mungu, lakini pia vipo vingine vinasababishwa na mazingira hasa kwa wajawazito au watoto wachanga. Mkimchagua Dk Magufuli nami nikawa makamu wa rais nitayatimiza hayo ya kuboresha mazingira," alisema Mama Samia.

No comments :

Post a Comment