dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, October 21, 2015

Vifaa vyote uchaguzi mkuu vifikishwe mapema vituoni!

NA EDITOR

21st October 2015.

Katuni.
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) imeeleza kuwa imekamilisha kazi ya kusambaza vifaa vya kupigia kura vitakavyotumika katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili ijayo.
 
Vifaa hivyo vimesambazwa katika mikoa yote ukiachia mikoa ya Pwani, Lindi, Mtwara na Dar es Salaam.
 
Tume hiyo imeeleza kuwa vifaa vya kupigia kura vitafikishwa kwenye vituo siku moja kabla ya upigaji kura.
 
Hatua iliyofikiwa na Nec ni ya kupongezwa kutokana na ukweli kuwa hadi sasa kazi iliyofanyika ni kubwa na tunategemea kazi ya kupeleka vifaa kwenye mikoa iliyobakia itafanyika haraka. Hata hivyo, pamoja na kazi nzuri ya Nec ya kuleta mapema vifaa vya kupigia kura nchini, lakini bado kuna changamoto ya kuwahisha vifaa kwenye vituo vya kupigia kura.
 
Mathalani, katika moja ya mikoa iliyotajwa kuwa bado haijasambaziwa vifaa vya kupigia kura ni Dar es Salaam.Hili jambo ni la kushangaza kidogo kwani iweje Nec  ishindwe kusambaza mapema vifaa jijini Dar es Salaam, ambako yalipo makao makuu ya tume hiyo.
 
Tunapendekeza kuwa vifaa hivi vigawiwe haraka mkoani Dar es Salaam ili kuhakikisha kuwa vituo vinakuwa na vifaa siku ya Jumapili. Tunahimiza jambo hili kwa kuwa tuna kumbukumbu nzuri ya kile kilichotokea kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 1995. Vifaa vya kupigia kura vilicheleweshwa kwenye maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dar es Salaam na kusababisha kusimamishwa uchaguzi kwenye maeneo hayo.
 
Matokeo yake uchaguzi huo ulirudiwa na kufanyika wakati matokeo ya kura za urais na wabunge wa sehemu nyingine nchini yakiwa yameshatangazwa. Pia ilitokea kwenye uchaguzi wa Zanzibar mwaka 2000 wakati masanduku ya kura yalipochelewa katika vituo mbalimbali vya Unguja. Hali hiyo ilisababisha kurudiwa kwa kura kwenye vituo mbalimbali vya mji wa Unguja.
 
Ni wazi kwamba uchaguzi wa mwaka huu unatazamiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na mwamko wa wananchi wa kushiriki kwenye uchaguzi huu.
 
Ushahidi wa jambo hili uko wazi kutokana na idadi kubwa ya watu wanaojitokeza kwenye mikutano ya kampeni.
 
Ushindani unatazamiwa kuwa kwenye uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani kutokana na njaa ya wananchi kutaka mabadiliko. Hata hivyo, ni jambo zuri kuona kuwa vyama vyote vimekuwa vikisisitiza kuwa vinataka kubadili maisha ya Watanzania. Sasa haitakuwa jambo zuri kwa Nec kuhusika kwa njia moja ama nyingine katika kuwanyima Watanzania nafasi ya kushiriki vizuri kwenye uchaguzi huu.
 
Ni kwa mantiki hiyo tunasisitiza itakuwa jambo zuri ikiwa vifaa vya kupigia kura vitapelekwa mapema kwenye vituo vya kupigia kura. Ukizingatia kuwa uchaguzi wa mwaka huu utakuwa na ushindani kwa hiyo bila shaka kila kura ni muhimu. 
 
Tunashauri Nec ikahakikisha masuala ya utawala yanakwenda vizuri ili kusiwapo na matatizo kwenye uchaguzi huu. 
 
Kutokana na ukweli kuwa yanapokuwapo matatizo ya utawala kwenye uchaguzi, ndiyo kwa kiasi kikubwa huchangia malalamiko. Kwa muda mrefu kumekuwa na dhana ya suala la wizi wa kura, sasa ili kuondoa wasiwasi huo, ni vizuri sasa kwa Nec kuhakikisha kuwa masuala ya vifaa vya kupigia kura yanatatuliwa.
 
Pia ukizingatia kuna idadi kubwa ya wapigakura iliyojitokeza kwenye uchaguzi huu, bila  shaka suala la kuwahi vifaa ni muhimu likatiliwa mkazo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment