Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, December 23, 2015

Jenista: Kukitokea maafa El Nino, kamati kuwajibishwa

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama.
By Julius Mathias
Dar es Salaam. Serikali imesema itawawajibisha wajumbe wa kamati za maafa watakaoshindwa kuchukua hadhari dhidi ya maafa yatakayosababishwa mabadiliko ya tabia ya nchi na mvua za El Nino kwenye maeneo yao.
Tamko hilo lilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama katika taarifa yake kwa vyombo vya habari baada ya mvua kuanza kusababisha madhara kwenye baadhi ya maeneo.
Madhara hayo ni pamoja na mafuriko, ukame na mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu.
Jenista, ambaye ofisi yake hushughulikia maafa, alisema kamati hizo za mikoa, wilaya, kata na vijiji zina jukumu la kuwaandikia barua wananchi wanaoishi maeneo hatarishi kuondoka mara moja ili kuepusha maafa hayo.
“Nawaagiza wenyeviti wa kamati za maafa kushirikiana na taasisi na idara za Serikali kuorodhesha watu wote wanaoishi maeneo hatarishi na kuwapa mara moja barua za kuhama. Taarifa za utekelezaji wa agizo hili ziwasilishwe Ofisi ya Waziri Mkuu haraka sana, kadri iwezekanavyo na kwenye vyombo vya habari,” alisema.
Alisema endapo kamati hizo zitashindwa kuchukua hatua, zitatakiwa kueleza sababu za kutokea kwa maafa kwenye maeneo yao na kuainisha hatua zilizochukuliwa kukabiliana nayo.
Alisema kamati hizo zitatakiwa kutoa maelezo ya kushindwa kutekeleza agizo hilo na kuainisha mipango ya kupambana na kipindupindu ambacho kimesambaa mikoani mbalimbali nchini na kusababisha vifo vya watu.
Ili kufikia lengo hilo, Jenista amezitaka kamati hizo kuendelea kuratibu na kutoa taarifa juu ya misaada inayotolewa na Serikali na wadau kwa waathirika kwa kuwashirikisha wananchi, taasisi za umma na sekta binafsi katika kudhibiti maafa.
“Kamati hizi kwa ngazi zote, zinatakiwa kumchukulia hatua mtendaji au mhusika ambaye hatatimiza wajibu wake na maagizo yanayotolewa na viongozi nchini kukabiliana na maafa mahali popote. Kamati zihakikishe zinatimiza wajibu kwa mujibu wa sheria,” alisema Jenista.
Agosti mwaka huu Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) ilitoa hadhari ya kuwapo kwa mvua za El-Nino, hivyo Serikali kuiagiza mikoa yote nchini kujiandaa kukabiliana na maafa yanayoweza kusababishwa na mvua hizo. Serikali imewaomba wadau wote wa maafa kutoa ushirikiano ili kuwaokoa wananchi wengi ambao wako hatarini.

No comments :

Post a Comment