
Rais wa Rwanda Paul Kagame.
Kigali.Rais wa Rwanda Paul Kagame amewataka raia wa nchi hiyo kuendelea kuwa na ujasiri na kujiamini wakati wa kufanya maamuzi yanayohusiana na mustakbali wa taifa hilo kwani wao ndiyo wenye dhamana ya kufanya hivyo.
Akizungumza katika majadiliano ya kitaifa yanayofanyika kila mwaka nchini humo Kagame alisema kwa nchi ilipofikia sasa hakuna sababu ya kukubali kuvurugwa na watu au nchi zisizoitakia mema Rwanda
Majadiliano hayo yanayofahamika zaidi kama ‘Umushyikirano’ yanafanyika kwa mara ya 13 mfululizo na mwaka huu yamehusisha watu zaidi ya 3000 wakiwemo wawakilishi wa nchi mbalimbali.
Alisema pamoja na kupokea ushauri na changamoto kutoka kwa watu wa nje lakini hawawezi kukubali ushauri unaolenga kuwatusi na kuwarudisha nyuma.
“Hatuna tatizo na washauri wetu kwani ushauri wao unaweza kuwa msaada lakini tunapoona wanavuka mipaka na kutuangalia ndivyo sivyo tunaachana nao na kuendelea na mambo yetu”alisema Kagame
Akizungumzia kura ya maoni ya mabadiliko ya katiba iliyofanyika Desemba 18 mwaka huu alisema matokeo ya kura hiyo yamedhihirisha wazi ni kitu gani raia wa Rwanda wanahitaji.
Alisema wananchi wa Rwanda wameonyesha jinsi demokrasia ya nchi hiyo ilivyokuwa na kukomaa ndani ya muda mfupi hali inayowafanya waendelee kujitathimi na kukataa kuvrugwa.
“Wanyarwanda wanatarajia utawala bora, hakuna mtu ambaye yupo kwa ajili ya kuongoza milele muda utakapofika wenyewe wanajua namna ya kubadilisha madaraka kwa njia ya amani na utulivu”
Aliongeza kuwa kwa kipindi cha miaka 21 nchi hiyo imeweza kupiga hatua kiuchumi na katika sekta mbalimbali matokeo ambayo yamekuja kufuatia jitihada za kila mmoja.
Tumeweza kuwa na mafanikio makubwa bila kutegemea msaada kikubwa ni kujitolea na wananchi kila mmoja kwa nafasi yake kutekeleza majukumu yake na tutaendelea kufanya hivyo”
No comments :
Post a Comment