Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 22, 2015

Kasi ya Rais Magufuli yafuta likizo TRA

Rais John Maguli
By Suzan Mwillo, Mwananchi
Dar es Salaam. Kasi ya Rais John Magufuli kuitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imewalazimu kufuta likizo kwa wafanyakazi wake wote ili kufikia malengo ya ukusanyaji wa mapato kwa kiwango cha juu.
Wakati uongozi wa mamlaka hiyo ukifuta likizo hizo, tayari Rais Magufuli ameipongeza kwa kukusanya mapato ya zaidi ya Sh1.3 trilioni mwezi huu. Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa mlipa kodi, Richard Kayombo alisema lengo ni kuhakikisha kuwa mapato zaidi yanakusanywa.
Hata hivyo, inaelezwa kuwa kufutwa kwa likizo hizo kutokana na mtikisiko ulioikumba mamlaka hiyo ukiwamo wa kuibuliwa kwa ufisadi katika ukusanyaji wa mapato uliosababisha watumishi 35 kuchukuliwa hatua mbalimbali, wanane kati yao wakifikishwa mahakamani akiwamo Kamishna wa Forodha, Tiagi Masamaki.
Wafanyakazi wa TRA wataungana na wenzao wa Tanesco ambao pia likizo zao zilifutwa na Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa lengo la kushughulikia tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa nishati hiyo nchini.
Mkoani Kilimanjaro nako, mkuu wa mkoa huo, Amos Makalla alipiga marufuku likizo za wakuu wa wilaya, wakurugenzi na wakuu wa idara kwenye mkoa wake ili kutekeleza kwa vitendo hotuba na maagizo ya Rais Magufuli.
Msimamo wa Tucta
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam Desemba 2, Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tucta), Hezron Kaaya alitaka ieleweke kuwa likizo ni haki ya mfanyakazi na kama kuna mwajiri anataka kuzuia likizo hiyo, anapaswa kufanya majadiliano na mwajiriwa ili wakubaliane kulingana na taratibu za sheria zilizopo. 

No comments :

Post a Comment