Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, December 22, 2015

Muhongo kutimua wazembe Tanesco

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo     
By Bakari Kiango, Mwananchi
Dar es Salaam. Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema ataanza kuwatimua wafanyakazi wazembe, wavivu na wasiokuwa na tija kwenye Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika muda wa siku 90 zijazo.
Pamoja na kuwataka watendaji wake kwenda na kasi yake ili asiwepo atakayeshindwa hivyo kulazimika kuachia ngazi, Profesa Muhongo ametoa maagizo matatu kwa Tanesco
Akizungumza juzi katika Kituo cha Somanga, Lindi wakati wa majumuisho ya ziara yake ya siku tano ya kutembelea vituo vya kuzalisha umeme kuanzia Hale mkoani Tanga, Nyumba ya Mungu mkoani Kilimanjaro Mtera (Dodoma), Kihansi (Iringa), Kidatu (Morogoro), Mamlaka ya Bodi ya Maji ya Mto Rufiji (Rubada), Somanga (Lindi) na mitambo ya gesi ya Madimba ya kuchakata gesi mkoani Mtwara, Profesa Muhongo alisema: “Siko tayari kubaki na wazembe. Afadhali nibaki na watumishi wachache wanaojituma. Sasa ifikapo Februari mwakani, mfanyakazi atakayebainika kashindwa kwenda na kasi yangu atalazimika kuitema nafasi ili ichukuliwe na vijana.
Maagizo matatu
Akiwa Somanga Profesa Muhongo aliamuru Tanesco kuwasha mashine zote zilizokuwa zimezimwa kwa ajili ya dharura ili zipeleke umeme katika maeneo yenye uhaba akisema wizara yake imedhamiria kumaliza tatizo hilo.
Agizo hilo lilitolewa baada ya kupewa taarifa na Meneja wa Somanga, Mhandisi Job Leonard kuwa kati ya mashine tatu za kituo hicho, moja ndiyo inafanya kazi, ya pili imepumzishwa; ya tatu inasubiri kufanyiwa matengenezo mwakani.
“Kila mara nawaambia Tanesco mmekosa ubunifu, mnajifanya mnabana matumizi huku Watanzania wanalalamikia umeme. Endapo mngewasha mashine iliyobaki si ingeweza kupeleka umeme katika gridi ya taifa ili tupunguze adha kwa wananchi?” alisema.
“Suala hili halipo hapa Somanga nimetaarifiwa hadi Biharamulo lipo. Huko nako nitakwenda kuangalia mitambo iliyowekwa bila kufanya kazi,” alisema Profesa Muhongo na akataka tatizo la mashine kutowashwa litatuliwe kuanzia wiki hii na waache visingizio vya kukauka kwa Bwawa la Mtera.
Agizo jingine alilolitoa ni kwa wakulima wenye mashamba makubwa kufungiwa maji ili yaelekezwe katika mabwawa ya kuzalisha umeme. Agizo hilo linatarajiwa kuathiri mashamba makubwa ya mpunga ya wawekezaji wa Kapunga na Mbarali, na wakulima wadogo wadogo wa Madibira.
Shamba la Kapunga linachukua asilimia 70 ya maji ya Mto Ruaha na Mbarali limechukua maji ya Mto Balali wakati Madibira wanatumia maji ya Mto Lyandembela, mito ambayo hutiririsha maji katika Bwawa la Mtera.
Katika agizo la tatu, Profesa Muhongo ametaka Tanesco na Shirika la Mandeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kukaa pamoja kujadiliana namna ya kumpatia umeme mwekezaji wa kiwanda cha saruji, Alhaji Aliko Dangote.
Alisema kiwanda hicho kimeshaanza uzalishaji wa sarujii lakini kimelazimika kukodi mitambo nje kwa ajili ya kuzalisha umeme, mbali na kuwa na mitambo inayohitaji gesi asilia na makaa ya mawe ili kujizalishia umeme wa megawati 75.
“Wakipatiwa makaa ya mawe au gesi watazalisha megawati 75, ambazo wataipa Tanesco 35 na wao kubaki na 45 kama wanavyohitaji,” alisema Profesa Muhongo.  

No comments :

Post a Comment