Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, December 11, 2015

Magufuli akata, aunganisha wizara

Rais Dk John Magufuli akiwa na viongozi wengine wa Serikali wakiondoka katika ukumbi wa mikutano baada ya kutangaza Baraza jipya la Mawaziri Ikulu Dar es Salaam jana. Picha na Ikulu
By Julius Mathias, Mwananchi
Dar es Salaam. Baada ya wiki sita za kusubiri kwa shauku, hatimaye Rais John Magufuli ametangaza baraza dogo la mawaziri lenye wizara 18 likiongozwa na mawaziri 19 na manaibu wao 15.
Rais Magufuli jana alibainisha sura zitakazoshika hatamu ya utawala wake kwa miaka mitano ijayo, huku akizisisitiza kufanya kazi ili kutimiza malengo na matarajio makubwa waliyonayo Watanzania.
Katika uundaji wa baraza hilo, Dk Magufuli ameunganisha baadhi ya wizara, huku akizihamisha baadhi kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu na kuzipeleka Ofisi ya Rais na nyingine kuziondoa kwenye kujitegemea na kuziingiza Ofisi ya Waziri Mkuu.
Katika kutimiza ahadi ya kupunguza gharama, licha ya kuunganisha wizara nyingi zipo baadhi zitakuwa na mawaziri, ila hazitakuwa na manaibu wao kama ilivyozoeleka.
Katika baraza hilo amejumuisha mawaziri saba waliokuwamo kwenye serikali ya awamu iliyopita, sura nyingi ni mpya.
Wizara ya kwanza kati ya zilizotangazwa jana ni Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Utumishi na Utawala Bora itakayokuwa chini ya mawaziri wawili; George Simbachawene kutoka Kibakwe, Mpwapwa, Dodoma na Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Angellah Kairuki, wakisaidiwa na Selemani Jafo, Mbunge wa Kisarawe mkoani Pwani.
Awali, Tamisemi ilikuwa Ofisi ya Waziri Mkuu, wakati ambao Ofisi ya Rais ilikuwa na waziri watatu; Utawala Bora, Mahusiano na Uratibu, na Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
Mabadiliko pekee yaliyofanywa katuka ofisi hii ni kupunguza idadi ya mawaziri, kutoka watatu hadi wawili na naibu mmoja.
Wizara nyingine ni Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira itakayoongozwa na January Makamba, Mbunge wa Bumbuli, Tanga atakayesaidiwa na Luhaga Mpina ambaye ni Mbunge wa Kisesa mkoani Simiyu.
Ameziunganisha wizara mbili za Muungano na Mazingira, zilizokuwa na mawaziri wawili na kuziweka chini ya waziri mmoja na naibu wake.
Katika Ofisi ya Waziri Mkuu, ipo Wizara ya Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu itakayoongozwa na Jenista Mhagama, Mbunge wa Peramiho mkoani Ruvuma akisaidiwa na manaibu waziri wawili, Mbunge wa Kuteuliwa ambaye ni mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Dk Abdallah Possi pamoja na Anthony Mavunde, Mbunge wa Dodoma Mjini. Wizara hii ina nyongeza ya Walemavu.
Wizara ya Sera na Uratibu wa Bunge ilikuwapo, lakini ile ya Kazi, Vijana na Ajira ilijitegemea. Dk Magufuli amewakumbuka walemavu na kuwapa uwakilishi wa kudumu.
Mabadiliko hayo yamepunguza idadi ya wizara zilizokuwepo katika Ofisi ya Waziri Mkuu zilizojumuisha; Sera, Uratibu na Bunge, Uwekezaji na Uwezeshaji na Tamisemi, zilizokuwa na mawaziri watatu na manaibu wawili.
Wizara ya nne ni Kilimo, Mifugo na Uvuvi, itakayokuwa chini ya Mwigulu Nchemba wa Jimbo la Iramba Magharibi na naibu William Ole Nasha kutoka Ngorongoro.
Ni muunganiko wa wizara mbili zilizokuwa na mawaziri wawili na manaibu wawili. Awali, ilikuwapo ile ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi.
Wizara nyingine iliyotangazwa jana ni ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano ambayo haina waziri.
Dk Magufuli alimtaja naibu waziri wake, Mhandisi Edwin Ngonyani kutoka Jimbo la Namtumbo mkoani Ruvuma.
Rais, pia ameunda Wizara ya Fedha na Mipango ambayo haina waziri wakati naibu waziri wake atakuwa Dk Ashatu Kijaji, mbunge wa Kondoa Vijijini mkoani Dodoma.
Awali, Wizara ya Fedha ilikuwa inajitegemea ikiwa na waziri mmoja na manaibu wake wawili. Kwa sasa naibu mmoja imeondolewa.
Rais, pia aliitangaza Wizara ya Nishati na Madini itakayokuwa chini ya Prof Sospeter Muhongo, Mbunge wa Musoma Vijijni , Mara naibu wake Dk Medard Kalemani, anayetokea Chato mkoani Geita.
Wizara hiyo haijarekebishwa, isipokuwa kupunguzwa kwa manaibu waziri kutoka wawili na kubakia mmoja.
Wizara nyingine ni Katiba na Sheria chini ya Dk Harrison Mwakyembe, Mbunge huyu wa Kyela , Mbeya haitokuwa na naibu waziri kama ilivyokuwa awamu iliyopita. Zipo wizara nne ambazo hazitakuwa na manaibu waziri katika utawala wa sasa.
Wizara hizo ni, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa ikiongozwa na Dk Hussein Mwinyi, Mambo ya Ndani ya Charles Kitwanga na Viwanda, Biashara na Uwekezaji chini ya Charles Mwijage.
Wizara hii imetokana na zilizokuwa wizara za Viwanda na Biashara, Uwekezaji na Uwezeshaji.
Kutakuwepo pia na Wizara ya Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa chini ya Dk Augustine Mahiga, Mbunge wa Kuteuliwa akisaidiana na Dk Suzan Kolimba wa Viti Maalumu kutoka Njombe.
Hiyo imeunganisha wizara mbili; Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa pamoja na ile ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na imebaki kwa William Lukuvi, Mbunge wa Ismani, Iringa akishirikiana na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula.
Wizara ya Maliasili na Utalii bado haijapata waziri, isipokuwa inaye naibu ambaye ni Mhandisi Ramo Makala, kutoka mkoani Ruvuma.
Nyingine ambayo haijapata waziri ni Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi ambayo inaye naibu , Stella Manyanya, mwakilishi wa Jimbo la Nyasa lililopo Ruvuma.
Hiyo imechukua najukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia.
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto chini ya Ummy Mwalimu, Mbunge wa Viti Maalumu, Tanga na naibu wake, Dk Hamis Kigwangalla, Mbunge wa Nzega Vijijini imeunganisha Afya na Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto.
Nyingine ni Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo chini ya Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye akisaidiwa na Anastazia Wambura, Mbunge wa Viti Maalumu kutoka Mtwara.
Pia, ipo Maji na Umwagiliaji chini ya Profesa Makame Mbarawa, Mbunge wa Kuteuliwa kutoka Zanzibar akisaidiwa na Isaack Kamwelwe kutoka mkoani Katavi.

No comments :

Post a Comment