- Watuhumiwa wanne, akiwemo Meneja wa Benki ya CRDB tawi la Chanika jijini Dar es Salaam, wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za unyang’anyi wa kutumia silaha katika tukio ambalo lilisababisha mauaji ya walizi wawili ambao ni askari wa Suma JKT.
Aidha, Polisi imesema imegundua kuwa watuhumiwa hao licha ya kufanya matukio ya ujambazi huwa pia wanajihusisha na vitendo vya kigaidi.
Uporaji huo uliotokea Desemba 8 na kusababisha walinzi wawili wa Suma JKT kupoteza maisha.
Kwenye tukio hilo, walinzi wengine wa kampuni ya ulinzi ya SGL walijeruhiliwa kwa risasi na majambazi hayo yalifanikiwa kupora mamilioni ya fedha kutoka matawi ya benki za CRDB na DCD.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi Kanda ya Maalum ya Dar es Salaam, Sulemain Kova alisema camera za CCTV ambazo zimefungwa kwenye benki zilizimwa kwa saa 24 jambo ambalo limewashangaza na kuona kwamba kulikuwa na njama za wahudumu wa benki hiyo.“CCTV ilizimwa kwa saa 24; tumemuuliza meneja wa benki ni kwa nini zilizimwa siku ya tukio hana majibu yoyote anayotoa na sisi tulishapatiwa taarifa kwamba kuna kitu pale ndani,” alisema Kova
“Kuna michezo imekuwa ikichezwa na wafanyakazi wa benki.
"Kama mnakumbka tukio la wizi wa Barclays… Meneja lifanya vikao na wezi na kuwaeleza kwamba wakifika wampige kibao kimoja, hivyo na kwa huyu meneja wa CRDB Chanika atakuwa kacheza mchezo kama ule.”
Alisema Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi wake kwa ajili ya kuwakamata wote waliohusika katika tukio hilo ili wachukuliwe hatua kali kwa mujibu wa sheria.
Kamishna Kova alisema katika tukio hilo, fedha zilizochukuliwa na majambazi hao zinafikia Sh. Milioni 20 zilizotolewa kwenye akaunti mbili za benki ya CRDB na DCD.
Kova aliwataka wafanyakazi wa benki kuwa waaminifu katika kazi zao kuhakikisha wanalinda siri za wateja wao na wasishiriki katika matukio ya wizi.
Aidha, Kova aliwatahadharisha tena wafanyabiashara pamoja na watu wengine kuacha tabia ya kubeba fedha nyingi kwa kuwa jambo hilo linawashawishi wahalifu.
Alisema kwa yoyote ambaye anajua anahitaji kubeba fedha nyingi, awasiliane na polisi ili apatiwe ulinzi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :
Post a Comment