
Dk. Kiloloma alisema hayo jijini Dar es salaam jana wakati akifungua kambi maalum iliyoandaliwa kwa ajili ua watoto wenye matatizo hayo itakayoanza kutoa huduma zake kuanzia leo.
Alisema kila mwaka watoto 4,800 huzaliwa wakiwa na matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi nchini, lakini ni 1,800 pekee wanaofikishwa kupatiwa matubabu.
“Watoto wanaobahatika kuja hospitali ni wale wanaookolewa na mama zao baada ya kukimbia vitendo hivyo, hii inatokana na imani potofu kuwa watoto wenye matatizo ya aina hii kama mikosi ndani ya familia,” alisema Dk. Kiloloma. Alisema kambi hiyo inayohusisha madaktari bingwa wa mishipa ya fahamu na mifupa, itawahudumia watoto 60 kwa kufanyiwa upasuaji.
Alieleza kambi hiyo iliyoandaliwa kwa pamoja na chama cha kusaidia watoto wenye saratani (FOCCT) itawahudumia watoto kutoka mikoa ya Morogoro na Pwani. Mkurugenzi huyo alisema ugonjwa huo husababishwa na upungufu wa madini ya folic acid kwa mama mjamzito wa muda wa wiki mbili hadi sita.
Alisema kama mzazi akigundua mapema tatizo hilo na kupewa tiba sahihi, kuna uwezekano wa mtoto akapona kabisa. “Mtoto akifanyiwa upasuaji na kuwekwa mirija ya kunyonya maji kichwani, anakuwa katika hali ya kawaida kama walivyo wengine,” alisema zaidi Dk. Kiloloma.
Makamu Rais wa FOCCT, Janet Manoni alisema tatizo hilo limeongezeka baada ya mama wajawazito kuacha tabia ya kula mboga za majani.
Aliwahimiza akina mama kupendelea kula vyakula hivyo kila mara ili kuepuka madhara yatakayojitokeza baada ya kuhifungua.
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment