Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, December 21, 2015

Polisi Zanzibar wamwangukia Rais Dk. John Magufuli

Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame
Askari wastaafu wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamemuomba Rais Dk. John Magufuli (pichani), kuingilia kati mkwamo wa malipo ya mafao yao tangu walipostaafishwa Julai, mwaka huu.
Wakizungumza katika Ofisi za Nipashe Kikwajuni Mjini Zanzibar juzi, baadhi ya askari hao walisema wamekuwa wakipigwa danadana kuhusu malipo yao na kuwafanya waishi katika mazingira magumu.
Askari hao ambao waliomba kuhifadhiwa majina yao, walisema wamejitahidi kufuatilia mafao yao Tanzania Bara baada ya kuona wamekuwa hawapati majibu muafaka kutoka kwa wakubwa wao Makao makuu ya Polisi Ziwani Mjini Zanzibar.
“Tumeisha kwenda hadi Tanzania Bara kufuatilia mafao yetu, bahati mbaya tunasikitika tumekuwa tunapigwa danadana wakati tunadai haki yetu,”alisema askari kanzu mmoja mstaafu.
Alisema yeye alianza kulitumikia Jeshi la Polisi mwaka 1971, lakini Oktoba 17, mwaka jana, alipokea barua ya kutakiwa kustaafu kwa lazima baada ya kufikisha umri wa miaka 55 kwa mujibu wa sheria.
Askari hao walisema walipewa likizo za siku 28 kuanzia Juni, mwaka huu na kutakiwa kikabidhi sare za Polisi, kadi za bima za afya na wategemezi wake pamoja na kulipa madeni katika maduka ya polisi kabla ya kuacha kazi rasmi Julai mosi, mwaka huu.
“Kamishina wa Polisi Zanzibar anakushauri uandike maombi ya kustaafu kazi kwa umri wa lazima kwa IGP kwa kujaza fomu za maombi na maombi hayo yafanyike katika kipindi cha miezi sita kabla ya tarehe ya kustaafu,” walinukuu sehemu za barua walizoandikiwa na Kamishina wa Polisi Zanzibar za Oktoba, mwaka jana.
Askari hao walisema pamoja na barua hizo kuwatakia kila la kheri na fanaka katika maisha yao mapya ya nje ya Jeshi bahati mbaya kheri hiyo wameshindwa kuipata na kushuhudia ukali wa maisha tangu kustaafu.
Hata hivyo askari hao walitaka kufanyike uchunguzi wa kina kutokana na kuwepo baadhi ya askari waliositaafu pamoja na kulipwa mafao yao huku wengine wakiendelea kupanda ngazi bila ya mafanikio. “Tunaomba rais wetu Magufuli hatusaidie hali mbaya tunashindwa kusomesha watoto wengine tunaumwa au wanataka tuwe majamabazi wakati tumetumikia taifa kwa uadilifu mkubwa kabla ya kustaafu.”alihoji Askari Mmoja kutoka Kisiwani Pemba.
Alisema kuwa baada ya kupokea barua za kustaafu walilipwa nauli za kuwawezesha kurudi katika maeneo wanayotoka lakini mpaka sasa hawafahamu lini watalipa mafao yao.
Walisema tangu kuibuka kwa mkwamo wa uchaguzi Mkuu wa Zanzibar, hali ya maisha imekuwa ngumu kutokana na mfumko  wa bei unaoendelea kujitokeza huku mafao yao yakiwa yamekwama kupatikana. Mbali na askari hao, pia maofisa zaidi ya 60 wamekwama kwa miaka minne kulipwa mafao ya malipo ya mkataba wa kazi wa miaka miwili baada ya kuongezewa muda kuazia Januari, mwaka 2010.
Walisema baada ya kustaafu waliongezewa muda mpaka Desemba mwaka 2011 na kujazishwa mikataba ya kazi utumishi Makao Makuu ya Polisi Zanzibar lakini wamefuatilia mafao yao muda mrefu bila ya mafanikio.
“Tuliambiwa mafaili yetu yametumwa Makao Makuu sasa mwaka wanne hakuna kitu lakini kuna watu wakipita katika njia za nyuma nyuma wanalipwa wakati tulistaafu pamoja.”alisema Askari mstaafu mmoja ambaye anasubuliwa na matatizo ya miguu.
Upande wake Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdan Omar Makame alithibitisha juzi kuwepo kwa askari wastaafu ambao bado hawajalipwa mafao yao.
Hata hivyo, alisema askari hao wanapaswa kuwasilisha malalamiko yao ofisini kwake ili afuatilie kujua mafao yao yamekwamia wapi badala ya kulalamika katika vyombo vya habari.
“Naomba sana waniletee malalamiko yao nipate kufuatilia na kuangalia mafao yao yamekwamia wapi,” alisema Kamishina Hamdan.
Alisema kuwa Jeshi la Polisi halipendi kuona askari wake wastaafu wakipata usumbufu na kuwataka askari hao kumpelekea mwenyewe malalamiko yao na atahakikisha yanafanyiwa kazi na kupatiwa ufumbuzi kwa wakati mwafaka.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment