Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, December 19, 2015

Profesa Muhongo aiagiza Tanesco ishushe bei ya umeme

Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo
Bei ya umeme inatarajia kushuka wakati wowote kuanzia sasa baada ya Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani chini)kuliagiza Shirika la Umeme (Tanesco), kushusha gharama za nishati hiyo.
 
Katika hatua nyingine, Waziri huyo amefuta likizo za wafanyakazi wa shirika hilo ili  washughulikie tatizo la umeme nchini huku akisisitiza kuwa hataki kusikia kukatika katika kwa umeme.
 
Profesa Muhongo alitoa maagizo hayo  jana jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika mtambo wa kuzalisha umeme wa Tegeta Gas Plant, ambapo alikwenda kwa ajili ya kukagua mitambo hiyo ili kuona kama yote inafanyakazi.
 
Akitoa maelezo ya mtambo huo, Meneja Mohamed Kisiwa alisema wana mitambo mitano na wana uwezo wa kuzalisha Megawati 42 kila saa.
 
Alisema gharama ya uzalishaji umeme kwa uniti moja ni Sh. 90 na wamekuwa wakiuza kwa Sh. 180 hadi 187.Profesa Muhungo alisema kwa maelezo ya meneja  huyo, inaonyesha umeme wanaozalisha wanapata faida mara mbili hivyo alisema kuna uwezekano mkubwa wa kushusha  gharama za umeme.
 
Aliagiza maofisa wa wizara yake na wa shirika la Tanesco wakutane leo ili wajue umeme huo utashushwa kwa kiwango gani.
 
 “Utauzaje umeme mara mbili ya gharama za uzalishaji,  tunataka kuwapunguzia wananchi bei ya umeme  na kwenye mkutano wetu wa kesho (leo) tutajadili  kupunguza bei ya umeme..haya mahesabu hayajakaa sawa maana unazalisha uniti moja kwa Sh. 90 na kuuza kwa Sh. 180 tutajadiliana mpunguze,” alisema.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment