AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, December 10, 2015

Rais Magufuli amefungua njia, suala la usafi liwe la kudumu

NA EDITOR

10th December 2015.

Watanzania jana walijitokeza kwa wingi kufanya usafi kuitikia agizo la Rais Dk. John Magufuli, la kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara kwa kufanya kazi hiyo.
 
Tukio hilo lilikuwa la kihistoria kutokana na mazoea yaliyojengeka kwa Watanzania kusherehekea siku hiyo kwa shamrashamra za gwaride la vikosi vya Majeshi ya Ulinzi na Usalama pamoja na halaiki.
 
Hata hivyo, Rais Magufuli kwa kuona kuwa Tanzania inakabiliwa na janga la ugonjwa wa kipindupindu akaelekeza watu wote wafanye usafi siku ya jana huku akiagiza fedha ambazo zilitakiwa kutumika kwa shughuli ya Uhuru, zielekezwe kwa ujenzi wa barabara.
 
Tunawapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kufanya usafi kwani wamedhihirisha mapenzi kwa nchi yao na uzalendo.
 
Pia pongezi zaidi ziende kwa viongozi wetu wakuu Rais Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na kwa wananchi kushiriki shughuli hiyo. Kitendo cha watu kujitokeza kwa wingi kufanya shughuli hiyo nchi nzima, kinadhihirisha kuwa Watanzania wana moyo na uzalendo wa kuitumikia nchi yao ila wanaangushwa na viongozi wao.
 
Jambo hili linadhihirisha kuwa kumekuwa na tatizo kubwa la usimamizi miongoni mwa watendaji wa serikali na ndiyo maana vijiji na miji yetu inakabiliwa na tatizo la uchafu.
 
Kujitokeza kwa wingi watu kufanya usafi, kunadhihirisha kuwa watu wana moyo wa kufanya kazi za kujitolea bali wanakosa hamasa kutoka kwa viongozi wao.
Ndiyo maana siyo ajabu kuona kuwa miji na vijiji vya nchi yetu vinakuwa na hali ya uchafu wakati wapo viongozi wenye dhamana ya kusimamia jambo hilo.
 
Jiji la Dar es linashika nafasi ya 12 kwa uchafu duniani kwa mujibu wa Jarida la Forbes la Marekani ambalo liliripoti matokeo ya utafiti wa taasisi ya Mercer Health and Sanitation.
 
Pia mwaka 2012, Jiji la Dar es Salaam lilikuwa linashika nafasi ya nane miongoni mwa miji michafu duniani kwa mujibu wa utafiti wa taasisi ya NYC Partnership.
 
Novemba, mwaka jana, wabunge waliilaumu serikali kwa kushindwa kusimamia suala la usafi katika Jiji la Dar es Salaam. 
 
Hata hivyo, chanzo cha uchafu katika miji na vijiji mbalimbali nchini limechangiwa na uongozi mbovu, rushwa, ufisadi na mipango mibovu.
Miji kama Dar es Salaam inazidi kukua, lakini hakuna mipango miji nchini na matokeo yake kunakuwa na ujenzi holela.
 
Matokeo yake yake limekuwa jambo la kawaida kulipuka kwa ugonjwa kama kipindupindu kutokana na kukithiri kwa uchafu.
 
Ugonjwa wa kipindupindu ni fedheha kubwa kutokana na ukweli kuwa unachangiwa zaidi na uchafu.
 
Nchi ambazo zimeweka misingi bora ya kutunza mazingira na usafi, zilishasahau tatizo la kipindupindu.
 
Kwa mfano kwa nchi kama Marekani kwa mara ya mwisho kukumbwa na ugonjwa huo ilikuwa mwaka 1911 wakati barani Ulaya ilikuwa mwaka 1875. 
 
Tunashauri Rais Magufuli aweke misingi itakayohakikisha watendaji watakaoshindwa kusimamia usafi wawajibishwe.
 
 Rais Magufuli sasa ameonyesha njia, viongozi wetu wanapaswa kuendeleza jambo hili kwa kuweka utaratibu wa kudumu kwa wananchi kushiriki katika shughuli za usafi.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment