.png)
Hoja hiyo inakuja huku serikali ikiendelea kubomoa nyumba za wakazi hao kwa madai kuwa wanaishi maeneo hatarishi ya mabondeni.
Wakizungumza na Nipashe jana, walisema miaka tisa iliyopita ,Mkakati wa Kurasimisha Biashara za Wanyonge (Mkurabita) uliidhinisha nyumba zilizobomolewa kuwa makazi rasmi na kupewa leseni zilizotumiwa kukopa na kulipa kodi. “Dar zilikusanywa zaidi ya Shilingi bilioni nne ambazo ni mapato kwa serikali. Waathirika wa mabondeni tulichangia pia. Hii ilikuwa ni sera ya Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ya kurasimisha maeneo ya biashara na kukusanya mtaji mfu kujenga uchumi,” alisema Arafat Cleofas, mmoja wa waathirika. “Maeneo haya yana leseni ambazo tunazisajili upya kila baada ya miaka miwili, iweje leo ni hatarishi? Haiingii akilini Serikali ya Rais John Magufuli inawabomolea wananchi nyumba ambazo zilitambuliwa rasmi na zinalipia kodi za makazi fedha zinazoendesha serikali, “ aliongeza.
Muathirika mwingine, Berbara Urio aliongeza: “Sisi tunatumiwa vibaya na serikali na wanasiasa waliotoa hati hizo na kutuwezesha kuwa na makazi.” “Miaka ya 1990, aliyekuwa Katibu Mkuu wa CCM, Horace Kolimba, aliruhusu na kuhimiza waliobomolewa kwenye bonde la Jangwani waendelee kujenga na wasihamishwe. Mbona chama na serikali vinatuyumbisha?” Alihoji.
Alisema wakati wa mvua za El - Nino 1997 hadi 1998, watu wengi walikufa na mali kuharibika na serikali kuwapa maeneo ya Tuangoma na Yombo Dovya ili waathirika zaidi ya 5,000 wahamishwe.
“Kutokana na uongozi mbaya, ufisadi na tamaa, viwanja hivyo viliporwa na mafisadi na viongozi, “ alidai Urio na kwamba haikuwa tofauti kwa waathirika wa mvua za 2011 waliopewa ardhi Mabwepande, lakini ufisadi ulivuruga zoezi hilo.
Baadhi ya viongozi wa serikali za mitaa wa eneo hilo (majina tunayo), waliitaka serikali kuchunguza ufisadi kwenye mradi wa kupanua Mto Ng’ombe na kuboresha makazi ya wananchi ulifanyika maeneo ya Kijitonyama na Sinza kwa gharama ya zaidi ya Euro milioni tano (sawa na Sh. bilioni 11.6) ukihusisha viongozi wa Wilaya ya Kinondoni.
“Vigogo walivumbua mradi ukagharimiwa na Shirika la Ubeligiji la BTC ili kupanua mto na kuweka matuta ya mawe Tandale Uzuri. Cha kusikitisha kazi hiyo haikukamilika na fedha zililiwa,” aliongeza.
Kuna baadhi ya madiwani wanawatumia wakazi waliovunjiwa
CHANZO: NIPASHE
No comments :
Post a Comment