Rais John Magufuli
Busega. Watoto wanaolelewa katika Kituo cha Bikira Maria kilichopo Lamadi mkoani Simiyu, wameiomba Serikali ya Awamu ya Tano kukomesha mauaji ya watu wenye ualbino kutokana na imani za kishirikina.
Mmoja wa watoto hao, aliyefahamika kwa jina moja la Minza alisema ili watu wenye ualbino waishi kwa amani, ni lazima Serikali iwapige waganga wapiga ramli kwa madai kuwa wamekuwa wakichangia kukatwa viungo vyao na na kufa.
Minza alisema hayo jana baada ya kutembelewa kituoni hapo na Mbunge wa Viti Maalumu (Chadema), Gimbi Massaba.
Akikabidhi sabuni, sukari, mafuta na juisi kwa watoto hao, mbunge huyo alisema ameamua kutoa msaada huo baada ya kuguswa jinsi ambavyo watoto hao wamekuwa wakiishi katika mazingira hatarishi, huku wakikosa malezi ya wazazi wao.
Akitoa shukrani, Mkurugenzi wa kituo hicho, Maria Hellena alisema kina watoto 54 wakiwamo wenye ualbino na ulemavu wa ubongo. Hellena aliyaomba mashirika na watu binafsi kujitokeza kuwapatia msaada watoto hao na kuwapunguzia changamoto zinazowakabili.
No comments :
Post a Comment