
By Mussa Mwangoka, Mwananchi
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo, Chala Wilgis Mbunda alitoa hukumu hiyo mwishoni mwa wiki iliyopita.
Alisema kwa mujibu wa Sheria ya Afya ya Mwaka 2009, Kifungu cha 53,54,55 (C) na 111 (1) (2), watalipa faini hiyo na kuchimba vyoo ndani ya siku saba tangu wahukumiwe.
Wakati huohuo; watu wengine 15 wamehukumiwa kulipa faini ya Sh30,000 au jela miezi mitatu kila mmoja kwa kosa la kuacha kuchimbva mashimo ya taka na vichanja.
Hata hivyo, watuhumiwa hao walilipa faini huku wengine wawili wakihukumiwa kuchapwa viboko baada ya umri wao kuwa chini ya miaka 18.
Hivi karibuni ugonjwa huo ulilipuka miezi kadhaa iliyopita katika mwambao mwa Ziwa Tanganyika na kuua watu zaidi ya 10.
Eneo hilo limekuwa likikumbwa na maradhi hayo, kutokana na jamii ya watu wake kutokuwa na utamaduni wa kutokuwa na vyoo bora.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga, Iddy Kimanta alinukuliwa hivi karibuni akisema Serikali imejikita kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora sambamba na matumizi sahihi ya vyoo hivyo.
No comments :
Post a Comment