Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 16, 2016

DC Mlingwa ataka msaada ugawanywe, apingwa

By Filbert Rweyemamu, Mwananchi 
Siha. Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro, Dk Charles Mlingwa amejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutaka vitanda vilivyotolewa na Benki ya NMB kwa Shule ya Sekondari ya Namwai vipelekwe shule nyingine zenye mabweni.
Kauli hiyo ilizua miguno kutoka kwa wanafunzi ambao shule yao haijakamilisha ujenzi wa mabweni.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bodi ya shule hiyo, Humphrey Nnko alisema jana kuwa wana mahitaji makubwa ya vitanda kwa kuwa Julai wanafunzi wa kidato cha tano wataanza masomo.
“Mkuu wa wilaya kama ulivyosema kuwa wanafunzi wa kike wapewe kipaumbele kukaa bwenini ili kuwapunguzia changamoto, naomba badala ya hivi vitanda kwenda katika shule ambazo tayari zina mabweni utumie ushawishi wako tupate mabweni kwa haraka,” alisema.
Akipokea vitanda 44, meza na viti vyake 70 vyenye thamani ya Sh20 milioni, Dk Mlingwa alisema:
“Haya madawati yatabaki hapa ila vitanda vitapelekwa shule nyingine za ndani ya wilaya yetu zenye mahitaji makubwa ukizingatia Namwai bado haijawa na mabweni.”
Alisema msaada uliotolewa una manufaa kwenye sekta ya elimu inayokabiliwa na changamoto nyingi.
Diwani wa Engarenairobi na Makamu Mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Patrick Kimario alisema vitanda hivyo vimetolewa mahususi kwa ajili ya Shule ya Namwai kutokana na ukosefu wa vitanda unaowakabili.
Meneja wa NMB Kanda ya Kaskazini, Salie Mlay alisema wameamua kuwekeza kwenye elimu kwa ajili ya kuwawezesha wanafunzi kusoma kwa bidii.
Alisema Taifa linahitaji wataalamu wengi watakaoitoa Tanzania ilipo na kuipeleka mbele kimaendeleo, hasa kielimu.
Mlay alisema mwaka huu benki hiyo inakusudia kuwa na shule za mfano zitakazotoa elimu ya ujasiriamali na utunzaji wa fedha ili kuibua chachu ya kuweka akiba.

No comments :

Post a Comment