Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 17, 2016

Jaji Mutungi aviasa vyama vya siasa kufuata sheria, kanuni.

Msajili wa Vyama vya Siasa, JaJi Francis Mutungi.
Msajili wa Vyama vya Siasa, JaJi Francis Mutungi, wanasiasa kufuata na kuheshimu katiba na kanuni za vyama vyao ili kuepuka migogoro.
Jaji Mutungi ameyasema hayo kwenye barua yake yenye kumbukumbu namba HA.322/362/01/103 aliyoviandikia vyama vya siasa jana.
“Nimeona ni vyema nitumie fursa hii kuviasa vyama vya siasa kuhusu hali hii, kwani hali hii ya kufanya mambo kiholela pasipo kufuata katiba na kanuni ikiachwa iendelee…italeta migogoro na mipasuko mikubwa,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Barua ya Jaji Mutungu imetolewa wakati taifa likisubiri kurejewa kwa Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar unaopingwa na vyama kadhaa vya siasa, kikiwamo Chama cha Wananchi (CUF).
Jaji Mutungi alisema, “…nimeandikiwa barua na kupata nakala kutoka kwa baadhi ya vyama kuhusu migongano ya wanachama na viongozi au viongozi wenyewe kwa wenyewe kuhusu kushiriki uchaguzi wa marudio Zanzibar.”
Alisema kwa hali hiyo, vyama vinapaswa kumtumia mtu mwenye mamlaka kuzungumzia masuala ya kisera na kitaifa kama ilivyo Uchaguzi Mkuu wa marudio visiwani Zanzibar.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment