Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 17, 2016

Kampuni 12 zadaiwa kodi ya Sh10 bilioni

Meya wa Manispaa ya Kionondoni, Boniface Jacob akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni mhasibu wa manispaa hiyo, Maxmilian Tabonwa. Picha na Said Khamis
By Bakari Kiango, Mwananchi bkiango@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Kampuni 12 zinazomiliki mabango makubwa ya matangazo ya barabarani katika Manispaa ya Kinondoni, zinadaiwa kukwepa kodi  ya  zaidi  ya Sh10 bilioni na kusababisha  manispaa hiyo kukosa mapato.
Meya wa manispaa hiyo, Boniface Jacob alisema jana kuwa kwa mwaka wa fedha wa 2015/16, Kinondoni imeazimia kukusanya zaidi ya Sh40 bilioni  kutoka  katika vyanzo mbalimbali  vikiwamo vikuu sita ambavyo vitakusanya zaidi ya Sh35 bilioni.
Alisema miongoni mwa nyanzo hivyo ni  ushuru wa mabango ambao walitarajia kupata Sh13 bilioni, lakini  hali ni tofauti kwani hivi sasa kampuni hizo zimeilipa manispaa hiyo Sh2.5 bilioni badala ya kiasi walichokusudia.
“Mkiona Kinondoni inalalamika haina fedha, mambo yenyewe ndiyo kama haya. Wamiliki hawa wa mabango wanashirikiana na baadhi watendaji kitengo cha matangazo kufanya uhuni huu,” alisema Jacob.
Alisema mchezo huu umebainika baada ya manispaa hiyo kuunda timu  tatu kutoka kampuni binafsi ambazo zilifanya uchunguzi wa mabango yaliyopo maeneo mbalimbali ya manispaa hiyo, na kwamba baadhi ya watumishi waliohusika na mchezo huo wameshachukuliwa hatua.
Alisema timu hizo tatu zimegundua udanganyifu wa aina mbalimbali unaofanywa na wamiliki wa mabango hayo, ikiwamo vipimo, ukubwa na idadi ya mabango hayo yaliyowekwa barabarani  kuwa tofauti na  vielelezo vilivyowasilishwa na kampuni hizo.
“Tungewatumia watumishi wa ndani kufanya uchunguzi huu ingekula kwetu. Lakini hizi timu tatu zimefanya kazi kubwa, kwa sababu hawa wamiliki wa mabango wanapiga fedha nyingi, ukiwa na bango moja Kinondoni unalipia Sh30 milioni tena kwa dola,” alisema Jacob.
Jacob ambaye pia ni Diwani wa Ubungo (Chadema), aliwapa siku saba wamiliki hao kulipa fedha hizo, kila mmoja kulingana na anavyodaiwa na baada ya hapo, hatua madhubuti zitachukuliwa dhidi yao, ikiwamo kushusha mabango  wanayoyamiliki.
“Tunahitaji hizi fedha walizokwepa kulipa  haraka iwezekanavyo ili tuzipeleke kwenye sekta ya elimu. Najua  kuna  wengine watazunguka mlango wa nyuma na  kwenda ngazi za juu kutafuta huruma, lakini nawaambia huko wanajisumbua bora waje  hapa ofisini  tena wakiwa na fedha zetu,” alisema Jacob.
Alisema amechoshwa na hali hiyo ya udanganyifu inayofanywa na kampuni hizo, huku akitolea mfano moja ya kampuni iliyotakiwa kulipa Sh2 bilioni kama kodi, lakini imelipa Sh500 milioni tu.
Mhasibu wa manispaa hiyo, Maximilian Tabonwa alisema lengo la kufanya hivyo ni kuhakikisha mapato yanakuwa kwa kasi katika manispaa hiyo na walianza kwenye mabango madogo kisha kuhamia kwenye makubwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Platnum Media, aliyejitambulisha kwa jina la Martin, alisema hawezi kuzungumza chochote kwa kitu kilichoandikwa au tetesi zilizosemwa na mtu fulani.
Hata hivyo, Jacob alisema hadi kufikia saa 10 jioni jana, wamiliki na wawakilishi wa kampuni sita walikwenda kujisalimisha katika ofisi yake juu ya sakata hilo.

No comments :

Post a Comment