Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Monday, February 15, 2016

Magufuli mwanamabadiliko au kinara kuimarisha mfumo uliopo?

Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma Mjini.
Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015, ulikuwa ni mojawapo ya uchaguzi mgumu kutokea katika historia ya Tanzania. 
 
Dk. John Magufuli, ambaye alikuwa mgombea wa CCM, alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 58 ya kura halali zilizopigwa.
 
Rais Magufuli alianza kuchukua hatua zilizotuma ujumbe wazi kwamba utawala wake hautakuwa wa mazoea.  
 
Kwa watu ambao wamekuwa wakitetea serikali iliyo safi kwa kupambana na rushwa hasa kubwa, Magufuli alikuwa ni kiongozi wa kukaribishwa.
 
Wengi wetu tulisherehekea hatua zake maarufu kama ‘kutumbua majipu’ na kufikia leo hii ninapoandika makala hii, zaidi ya watu 150 wamefukuzwa ama kusimamishwa kazi.
 
Wengi wa waliokumbwa na dhahama hii wanatoka bandarini na Mamlaka ya Mapato (TRA). Mafanikio aliyoyapata kwenye mwezi wake wa kwanza akiwa madarakani ni pamoja na ongezeko mapato ya serikali.Rais Magufuli alitoa hotuba yake ya kwanza bungeni iliyosisitiza kwa kiasi kikubwa mapambano dhidi ya rushwa, kupunguza matumizi yasiyo ya lazima ya serikali na kuongeza mapato na sekta ya uchumi wa viwanda. Akawa ni mtu wa kuzungumzwa katika kanda hii na wakati mwingine katika anga za kimataifa.  
 
Jalida la The Economist, lilitoa makala maalumu kulinganisha kupanda kwake kwenye vyombo vya habari na vya kijamii. Je utawala wake wa siku 100 umemtafsiri yeye ni kiongozi wa aina gani? Je tunaweza kumuita kama kiongozi mwanamabadiliko?Je mwanamageuzi?Je ni kinara wa kuimarisha mfumo uliopo?
 
Archie Brown, kwenye kitabu chake cha semina, The Myth of the Strong Leader, anamuelezea  kiongozi mwanamabadiliko kama ‘yule mwenye jukumu la maamuzi kwenye kuanzisha mabadiliko yaliyo na utaratibu’ kama ni ya mfumo wa kisiasa au wa kiuchumi kwa nchi yake. 
Kinapendekeza mabadiliko makubwa, lakini ya ujenzi wa msingi wa mfumo ulio bora kuliko uliokuwapo kabla’.
 
Inaweza kuwa ni mapema mno (siku 100 tu) kumtafsri Rais Magufuli, hata hivyo siku 100 za kwanza zinaweza kutusaidia kuona Rais Magufuli atakuwa kiongozi wa aina gani.
 
Magufuli alichukua madaraka na ahadi ya mabadiliko. Wapinzani wake waliahidi mabadiliko pia. 
 
Kundi la kisiasa lililokuwa likiongoza upinzani lilikuwa na ujumbe wazi kwamba, lilitaka kubadilisha mfumo na mara kwa mara lilirejea ‘mfumo wa rushwa’ au rushwa ni utaratibu.
 
 Je, hatua za Rais Magufuli dhidi ya rushwa zina mfanano wowote na kuuvunja mfumo wa rushwa?
Amewafukuza watu kazi na kuwashtaki baadhi yao mahakamani.
 
Na hata amemfukuza kazi aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk. Edward Hosea. 
 
Tumeona watu wakiondolewa kwenye nyadhifa zao na wengine wakibadilishwa na kuwekwa.
Je, Takukuru na wakala zingine za uwajibikaji zimebadilika?
 
Haya ndiyo maswali muhimu na ya msingi sana ya kumchambua Rais Magufuli.
 
Kimsingi, mfumo wetu umeambatana na kinga. 
 
Hatua za Rais Magufuli zimeonyesha kwamba kila mtu lazima aishi kwa mujibu wa sheria.
 
Hata hivyo, hajafanya chochote cha kugeuza mashirika yanayodumisha utawala wa sheria na kutekeleza sheria.
 
Takukuru bado ni ile ile. Bado haina mamlaka ya kushtaki bila ya idhini ya Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP). 
 
Katika siku zake 100, si kwamba Rais Magufuli amekuwa kimya kuzifanyia mageuzi taasisi, lakini pia tumeona vikao viwili vya Bunge vikiwa havijapitisha sheria yoyote kwa dhumuni hilo.
 
Kubadili wakuu wa taasisi hizi kunamaanisha Rais anapendelea kuuimarisha mfumo uliopo, kuliko kuubadilisha mfumo ambao ndio uliomuingiza yeye madarakani.
 
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment