Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, February 17, 2016

MAONI: Maridhiano hayaepukiki mpasuko wa kisiasa Zanzibar



By Peter Elias, Mwananchi
Mpasuko wa kisiasa Zanzibar umebaki kuwa fumbo kubwa baada ya Rais John Magufuli kutangaza kwamba ataendelea kukaa kimya kwa sababu hawezi kuiingilia Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC).
Kwa muda mrefu kumekuwa na shinikizo la watu mbalimbali kumtaka Rais Magufuli kutumia mamlaka yake kuingilia kati mgogoro wa kisiasa wa Zanzibar ulioanza baada ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi, Oktoba 28, mwaka jana.
Hata hivyo, Rais Magufuli alisema wakati akiongea na wazee wa Dar es Salaam kwamba Katiba haimruhusu kuingilia uamuzi wa ZEC kwa sababu Tume ya Uchaguzi ni huru na kwamba tayari imeshatangaza tarehe ya uchaguzi wa marudio.
Wakati uchaguzi huo ukitarajiwa kufanyika Machi 20, mwaka huu, tayari Chama cha Wananchi (CUF) kimesisitiza kutoshiriki ili kupinga kile wanachokiita kunyang’anywa ushindi wao.
Vyama vingine 10 vimetangaza kutoshiriki katika uchaguzi huo kwa madai kwamba wakishiriki watakuwa wamehalalisha maovu yaliyofanywa na Mwenyekiti wa ZEC, Jecha Salum Jecha.
Mgogoro huo wa kisiasa umeingia sura mpya baada ya vyama vingi vilivyoshiriki uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka jana kujitoa kushiriki uchaguzi huo ili kuwaunga mkono wenzao wa CUF ambao wanaaminika walishinda katika hatua za awali za uhesabuji wa kura.
Kutokana na sintofahamu hiyo, ninaamini kwamba Zanzibar inahitaji njia ya maridhiano ili kumaliza kabisa mtanziko wa kisiasa visiwani humo. Wadau wakuu katika maridhiano hayo ni pamoja na vyama vyote vya siasa vilivyoshiriki kwenye uchaguzi wa Oktoba, ambavyo ndiyo vina sifa ya kushiriki pia uchaguzi wa Machi 20.
Wadau wengine ni Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, kamati maalumu ya usuluhishi au msuluhishi mwingine kutoka jumuiya za kimataifa ambaye hafungamani na upande wowote.
Tumeona mazungumzo ya watu sita yaliyokuwa yakifanyika kushindwa kufikia mwafaka kwa sababu kila mmoja alikuwa akivutia upande wake. Mazungumzo hayo yalihitaji mtu wa katikati ambaye atasikiliza hoja za pande zote mbili, kupima uzito wake na kufanya maamuzi.
Ikumbukwe kwamba Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK)iliundwa kumaliza tatizo la kisiasa ambalo lilijitokeza baada ya uchaguzi wa mwaka 2000 na kusababisha ghasia mauaji ya watu na wengine kwenda uhamishoni.
Hata uchaguzi ukifanyika kwa mara ya pili na mshindi akapatikana bado maridhiano kati ya vyama vyenye ushindani mkubwa vya CCM na CUF yatahitajika ili kuondoa migogoro kati ya wananchi wanaounga mkono vyama hivyo.
Tayari Jumuiya ya Kimataifa kwa maana ya waangalizi wa kimataifa na mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao hapa Tanzania wameeleza kusikitishwa kwao na hatua ya kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar.
Wametoa wito wa kufanyika kwa maridhiano na mshindi kutangazwa ili Taifa livuke salama katika kipindi hiki cha sintofahamu. Bado zinahitajika jitihada za pamoja katika kusimamia upatikanaji wa maendeleo.
Taifa linapata hasara kubwa kuendelea kuishi katika hali ya sintofahamu iliyopo Zanzibar, kwanza ni kushuka kwa uzalishaji. Wananchi wengi wanashindwa kuzalisha kwa wingi kwa sababu ya hofu ya kiusalama inayoweza kuharibu biashara zao.
Hasara nyingine ni kupungua kwa watalii nchini au baada ya uchaguzi kwa sababu ninatambua hata uchaguzi ukifanyika bado makovu yatabaki.
Peter Elias ni mwandishi wa gazeti hili. pelias@mwananchi.co.tz au 0763891422.    

No comments :

Post a Comment