Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 16, 2016

Timuatimua watumishi wa umma yahamia TBC

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Clement Mshana baada ya kumaliza kikao na uongozi wa shirika hilo Dar es Salaam jana. Picha na Frank Shija


By Vicky Kimaro, Mwananchi
Dar es Salaam. Timuatimua inayofanywa na mawaziri wa Serikali ya Awamu ya Tano imehamia Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) baada ya viongozi wawili waandamizi kusimamishwa kazi kwa kile kilichoelezwa kuwa ni utendaji mbovu.
Waziri wa Habari, Nape Nnauye alitangaza jana kuwasimamisha kazi Mkurugenzi wa Idara ya Habari na Matukio, Mbwilo Kitujime na Meneja wa Vipindi, Edna Rajab.
Akizungumzia hatua hiyo, Nape alisema jana kuwa kumekuwa na mlolongo wa matuko mengi ndani ya shirika hilo ambayo yanakwenda kinyume na taratibu.
“Mbali na kuwasimamisha, nimeagiza kufumuliwa kwa idara nzima ya habari na matukio ya TBC kutokana na utendaji usioridhisha,” alisema na kuongeza: “Kwa vile suala lao linahusu bodi, nimeagiza bodi ichukue hatua zaidi kutokana na mlundikano wa mambo mengi.”
Waziri Nape alisema pia Bodi ya TBC inayoongozwa na Profesa Mwajabu Posi itateua watumishi wengine kukaimu nafasi zilizoachwa wazi na viongozi hao. “Unajua ni lazima tuelezane ukweli, kuna mlundikano wa mambo  mengi yanayofanyika ndivyo sivyo TBC, yaani ni mengi, sitaweza kutaja mojamoja, kifupi niseme tu utendaji hauridhishi, hali inayodhoofisha shirika.

Kutimuliwa kwa wakurugenzi hao ni mwendelezo wa kasi ya Rais John Magufuli ambaye tangu ameingia madarakani, yeye na mawaziri wake wamekuwa wakiendeleza falsafa ya kutumbua majipu, kiasi cha kuwaweka matumbo joto watendaji wa taasisi na idara mbalimbali za Serikali.
Kutimuliwa kwa mabosi hao, kumekuja baada ya kikao cha Waziri Nape na Bodi ya TBC kilichofanyika Januari 13 kuzungumzia changamoto mbalimbali zinazolikabili shirika hilo na jinsi ya kuzitatua.
Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Mkuu TBC, Clement Mshana alisema watatekeleza maagizo hayo ya waziri na kuwataka watendaji wengine wa TBC kufanya kazi kwa bidii.

No comments :

Post a Comment