Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, February 16, 2016

Waukubali utafiti uliompaisha Lukuvi

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi
By Kalunde Jamal, Mwananchi 
Dar es Salaam. Wadau wamekubaliana na matokeo ya utafiti yanayoonyesha kuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi anakubalika na wengi kutokana na utendaji wake kwenye Baraza la Mawaziri la Rais John Magufuli.
Walioa maoni yao kuhusu utafiti uliofanywa na kampuni ya Ms InfoTrak Research and Consulting & Ms Midas Touché East Africa Limited kwa ufadhili wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited, ulioonyesha kuwa Lukuvi alipata asilimia 13.1 ya watu wote waliohojiwa huku Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi akipata asilimia 2.0.
Maoni ya wananchi
Akizungumzia utafiti huo, mbunge wa Kigoma Mjini (ACT -Wazalendo), Zitto Kabwe alisema kulingana na dhana nzima ya kuinua uchumi na kuongeza ajira, alitegemea katika utafiti huo angewaona pia watu kama Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage; na Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Mifugo, Mwigulu Nchemba wakiongoza, lakini badala yake wameongoza wale wanaofanya kazi na wananchi kutatua kero zao.
Alisema katika utafiti huo yameainishwa mambo kadhaa kama elimu, afya, ajira, kukuza uchumi, kilimo na hao walioongoza ni wale wanaoonekana wakienda kwa wananchi na kutatua kero zao.
“Matatizo ya wananchi ni ardhi. Lukuvi amekuwa akienda kutatua migogoro mbalimbali ya ardhi. Pia, Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako ana haki ya kupata hiyo nafasi kwa sababu utendaji wake tangu akiwa Katibu wa Baraza la Mitihani ulikuwa unaonekana,” alisema.
Tangu ateuliwe kuongoza wizara hiyo, Lukuvi amekuwa akishughulikia mashamba yaliyomilikishwa kwa wawekezaji wa ndani na nje na ameshatangaza kufutwa hati za mashamba matano makubwa, huku akizuia uuzaji, wakati Dk Ndalichako amefuta  mfumo wa kupanga matokeo ya kidato cha nne kwa kutumia GPA na kurejesha wa madaraja.
Katika kipindi hicho, Dk Mwinyi ndiye ambaye hajaonekana kufanya shughuli nyingi zaidi ya kuhudhuria mahafali ya Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi ya Monduli, akiwa na Rais Magufuli.
“Kuhusu Hussein Mwinyi ni nadra sana wananchi kusikia masuala ya Waziri wa Ulinzi, kwa sababu ni ya kijeshi hivyo wanayafanya ndani kwa ndani,” alisema Zitto.
Mkurugenzi mtendaji wa Shirika la Sikika, Irinei Kiria alizitaja sababu za Lukuvi kuongoza na Hussein Mwinyi kuwa wa mwisho kuwa ni kutokana na utofauti wa wizara zao.
Alisema vitu anavyofanya Lukuvi vinaripotiwa na vyombo vya habari. Pia, anakwenda moja kwa moja kuonana na wananchi wa mijini na vijijini kutatua kero zao, kitu ambacho ni nadra kufanywa na Waziri wa Ulinzi.
Alisema Lukuvi amekuwa kifua mbele katika masuala mengi yanayohusu jamii moja kwa moja, likiwamo suala la ufukwe wa Coco, bomoabomoa na migogoro ya ardhi.

No comments :

Post a Comment