Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 12, 2016

Karatasi za Kura kwa ajili ya Uchaguzi wa Marudio Zawasili leo Mjini Unguja.




 Picha za ujio wa Makatarsi na huyo anayeonekana hapo ni Mkurugenzi wa ZEC  Salim Kassim Ali akitoa maelezo ya kuwasili kwake uwanja wa ndege Zanzibar.















Karatasi za kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio, zimewasili leo mjini zanzibar huku picha za wagombea wote 14 wa urais wa vyama vilivyoshiriki uchaguzi wa oktoba 25 mwaka jana zikiendelea kubaki kama zilivyo.

Mfano wa Karatasi ya kupigia kura
Karatasi hizo zimewasili katika uwanja wa ndege wa abeid amani karume mnamo saa nane na dakika saba mchana.

Mkurugenzi wa tume ya uchaguzi zanzibar salum Kassim Ali, amesema karatasi hizo zimegharimu shilingi bilioni nne na milioni tano ikiwa pungufu kulinganisha na karatasi za uchaguzi wa mwaka jana zilizogharimu shilingi bilioni tano na milioni tatu.

Aidha Mkurugenzi huyo, ameitaja kampuni ya Uniprint of Durban ya afrika kusini, kuwa ndio iliyochapisha karatasi hizo, na kwamba fedha zote zilizotumika kugharamia zoezi hilo zimetoka kwa serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Hata hivyo ameeleza kuwa vifaa hivyo vitaanza kusambazwa katika wilaya zote za unguja na pemba hapo machi 18, ili wananchi waweze kupiga kura ili kutoa fursa kwa wananchi wote kushiriki kwenye zoezi hilo.

Ametaja idadi ya karatasi hizo kuwa ni laki tano, elfu tatu, mia nane na hamsini kutokana na idadi ya wapiga kura kwa vituo 1,583 vya zanzibar.

Walioshiriki katika kuzipokea karatasi hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Jecha Salim Jecha, Mkurugenzi wa ZEC, Salim Kassim Ali, Makamishna Haji Ramadhani Haji, Omar Ramadhan Mapuri pamoja na Salmin Senga.


Kwa upande wa vyama vilivyoshiriki katika kupokea karatasi hizo ni pamoja na CCM na TADEA.

No comments :

Post a Comment