- Mbunge wa Newala Mjini (CCM) mkoani Mtwara, George Mkuchika, amepingana na sehemu ya taarifa iliyowasilishwa kuhusiana na sekta ya kilimo katika kikao cha Baraza la Ushauri la Mkoa wa Mtwara (RCC) inayoeleza kuwa sherehe za unyago hazina ulazima kwani zinachangia matumizi mabaya ya chakula.
Mkuchika alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), wakati wa utawala wa awamu ya nne ya Jakaya Kikwete.
Akizungumza mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuchika alisema kipengele hicho kimemchefua kwa sababu kila kabila katika nchi hii lina mila na desturi zake, hivyo siyo vizuri kukosoa mila za kabila pasipo kujua faida zake.
“Jandoni kuna elimu na hata baba wa taifa aliwahi kuelezea umuhimu wake… leo nyinyi mnakejeli, kulikoni,” alisema na kuongeza:
“Leo mmekuja kuleta mada hii wakati mnajua hapa kuna Wamakuwa, Wayao, Wamakonde na Wamwela ambao wana mila na desturi za unyago... naombeni sana, mtukome na mtuache,” aliongeza Mkuchika.
Alitumia muda mrefu kuwaeleza wajumbe wa kikao hicho mambo mbalimbali yanayohusu jando na unyago na kusema katika makabila ya Mtwara na Lindi,watoto wanapitia katika hatua zaidi ya tano wanapokuwa kwenye jando ikiwa ni pamoja na kupewa mafunzo juu ya maisha ya ndoa.
“Mtoto anatoka jandoni anaambiwa ni marufuku kwenda chumbani kwa baba na mama… ndiyo maana ukigombana na mdogo wako ambaye hajaenda jandoni anakimbilia chumbani kwa baba na mama. Ni kwasababu anajua wewe ulipitia jando huwezi kwenda kule,” alisema.
Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego, alimshukuru Mkuchika kwa maelezo yake na kusema kuwa kwa kiasi kikubwa, makabila mengi hapa nchini yana taratibu zinazofanana na kwamba wale ambao hawazifuati madhara yake wanayajua.
“Nafikiri ni mwandishi tu aliteleza kuliweka vizuri. Kuna shughuli zingine tunazifanya kwa kusherehesha ambazo zinasababisha kaya kuingia kwenye njaa pasipo sababu za msingi… lakini sidhani kama yupo mtu mzima hapa atadharau maana ya jando na unyago.
Na watoto wetu wanakosa mengi ndiyo maana wanapungukiwa kwenye mengi, lakini kwa wengine ambao tumepita huko tunaelewa maana yake Mheshimiwa. Kwa hiyo tuko pamoja,” alisema.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments :
Post a Comment