zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 6, 2016

Mama auawa kwa mapanga akipalilia mpunga

Image result for killing by machetes

  • Mwanamama aitwaye Sofia  Mussa (65) wa Kijiji cha Tulieni kilichopo katika tarafa ya Nakapanya, Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma, amefarika dunia katika tukio la kushambuliwa kwa mapanga.

Baadhi ya mashuhuda wa mwili wa marehemu wamesimulia kuwa kabla ya kifo chake, marehemu alikuwa shambani kwake akiendelea na kazi ya kung'olea mpunga.

Diwani wa Kata ya Nakapanya, Kubodola Ambali, alisema kuwa tukio hilo lilitokea Alhamisi, majira ya saa 3:00 asubuhi baada ya mama huyo kuvamiwa na watu hao wasiojulikana wakati akiwa shambani kwake.

Akizungumzia tukio hilo, mume wa marehemu, Sheikh Athuman Mohamed, alisema siku ya tukio, marehemu alikwenda shambani akiwa peke yake.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mombeji, amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi.

Alisema kufuatia tukio hilo, jeshi hilo linamshikilia mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Alifa Haji (30) kwa ajili ya kumhoji na kwamba, ikibainika kuwa ni miongoni mwa washiriki wa tukio hilo atafikishwa mahakamani.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment