zanglassworks

AirFreight

Kwarara Msikitini

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Sunday, March 6, 2016

Mkurugenzi afariki siku moja kabla ya Majaliwa kumkagua

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu, Trasia Kagenzi,
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa Mkoa wa Simiyu, Trasia Kagenzi, amefariki dunia ikiwa ni siku moja tu kabla ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kukagua miradi ya maendeleo ya wilaya yake.

Habari za uhakika zilizopatikana wilayani humo zilisema kuwa Kagenzi alifariki dunia jana kwa ugonjwa wa shinikizo la damu, wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya rufaa ya Bugando, Mwanza.

“Alijisikia vibaya tu ghafla na watu aliokuwa nao walimkimbiza hospitali ya Bugando kwa matibabu lakini alifariki muda mfupi baadaye,” kilisema chanzo hicho.

Leo asubuhi, Waziri Mkuu alipangiwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ya Wilaya ya Maswa inayotekelezwa kwa usimamizi wa Kagenzi.

Baadhi ya miradi hiyo ni pamoja na ule wa ujenzi wa chujio la bwawa la Zanzui na kufungua jengo la wagonjwa wa nje katika hospitali ya wilaya.

Majaliwa pia alipangiwa kukagua ghala la kuhifadhia chakula la Malampaka na kisha kufanya mkutano wa hadhara wilayani Maswa.
Kufuatia kifo hicho, habari zilisema kuwa Waziri Mkuu hatakagua miradi hiyo ya Maswa na badala yake atafanya majumuisho ya ziara yake katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Maswa.

Mwandishi waHabari wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Irene Bwire alikiri kutokea kwa msiba huo na kueleza Majaliwa hatafanya ziara kwenye wilaya hiyo kama ilivyopangwa.

“Ziara haitafanyika tena Maswa badala yake mheshimiwa ataenda msibani kesho asubuhi na baada ya hapo atafanya majumuisho ya ziara yake nzima,” alisema Bwire.

Majaliwa alifanya ziara katika Wilaya za Busega, Bariadi, Bariadi Mjini, Itimila, Meatu.

Juzi akiwa Itilima, Majaliwa, aliwakumbusha watumishi wa umma kwamba atakayeharibu kazi atafukuzwa hapohapo alipo na hakutakuwa na uhamisho.

Alisema watumishi wa umma wako huru kuhamia kokote wapendako lakini wahakikishe wanaenda huko wakiwa safi na kamwe mtu asiharibu kazi akitarajia kuwa atahamishiwa sehemu nyingine.

"Serikali hii haina utumishi kwa mtu aliyeharibu kazi… usije ukaharibu hapa Itilima ukadhani utaenda Bunda kuendelea na kazi, serikali ya awamu hii haina nafasi na  watumishi wa aina hiyo," alisema.

"Watumishi wenzangu huu ni wakati wa kubadilika na kuona mwelekeo wa Serikali hii ya awamu ya tano ukoje, jukumu letu ni kuwatumikia Watanzania wote bila kujali itikadi zao, rangi wala dini zao."
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

No comments :

Post a Comment