Tukio hilo lilitokea Machi 22, jioni katika Kijiji cha Swaila wilayani Nkasi.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo alikimbia nyumbani kwao na kwenda kujificha porini baada ya mama yake kumtishia kumpeleka ofisi ya Serikali ya kijiji akafungwe kwa kumiliki simu ya mkononi ambayo hajui alikoipata.
Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Swaila, Juvenary Mmanzi alisema mama huyo alishangaa kuona mwanaye huyo wa kike akiwa na ‘smart phone’ ambayo hata yeye hana uwezo wa kuinunua.
Alisema akiwa porini, mvua ilianza kunyesha hali iliyomlazimu arudi kijijini kujikinga, hivyo alipokuwa njiani, alipigwa na radi na kufa papo hapo.
Baada ya watu kufika eneo alikopigwa radi mtoto huyo, walikuta mwili wake umeungua na kwenye mfuko wa sketi aliyokuwa ameivaa kukiwa na simu hiyo aina Tecno.
Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, Jacob Mwaruwanda aliwaasa wananchi kuacha kujificha au kujikinga mvua chini ya miti au porini ili kuepuka ajali ya kupigwa na radi.
No comments :
Post a Comment