Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, March 25, 2016

Tanzania yafafanua kuzuiwa waziri wa Kenya kuingia bandari ya Tanga

Waziri wa Nishati wa Kenya, Cherles Keter.

Waziri wa Nishati wa Kenya, Cherles Keter, na ujumbe wake amezuiwa kuingia katika bandari ya Tanga.
Kutokana na hatua hiyo, serikali mkoani Tanga imetoa ufafanuzi kuhusu kuzuiwa kwa waziri huyo na ujumbe wake wa watu 13 kuwa kulitokana na kutokuwa na taarifa za ujio wao.
Keter na maofisa wake wandamizi wakiwamo makatibu wakuu, walijipenyeza wakati wa ziara ya Waziri wa Nishati na Madini wa Uganda, Irene Muloni.
Ujumbe wa waziri huyo aliyeongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati ya nchi hiyo, Joseph Njoroge na mwenzake wa masuiala ya petroli, Andrew Kamau.
Vigogo hao, waliokuwa wameongozana na maofisa mbalimbali akiwamo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Usafirishaji wa Mafuta kutoka Lamu- Sudan Kusini- Ethiopia (Lappset), Sylvester Kasuku, walizuiwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Tanga, baada ya kuwasili. 
Muloni na ujumbe wake, alitokea Kenya baada ya kukagua Bandari za Lamu na Mombasa na aliingia nchini kukagua Bandari ya Tanga, ikiwa hatua ya mchakato wa ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta kutoka Ziwa Albert, Uganda hadi Bahari ya Hindi.
Mpaka sasa serikali ya Uganda iko katika mchakato wa ukaguzi wa Bandari za Lamu, Mombasa kwa upande wa Kenya na Tanga kwa upande wa Tanzania ili kupata bandari itakayokidhi vigezo vya kuendesha mradi huo.
Akizungumza hatua hiyo, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa wa Tanga, ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa, Martin Shigella, alisema ujumbe wa Keter ulizuiwa kutokana na kutokuwa na taarifa nao na kwamba walikuwa katika viwanja vya ndege kwa ajili ya kungoja ugeni wa Waziri Muloni tu.
Shigella alisema kuwa walishangazwa kuona ujumbe huo wa Kenya umekuja kufuatana na waziri huyo bila kuwapo kwa taarifa yeyote ya awali ya ujio wao.
Keter na maofisa wake waliwasili katika uwanja wa ndege wa Tanga sambamba na ujumbe wa Waziri wa Uganda, ambao wote kwa pamoja waliwasili kwa helikopta nne, zilizotua kwa pamoja uwanjani hapo.
Baada ya kuhojiwa na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na baada ya Waziri Muloni kumaliza ukaguzi wa Bandari ya Tanga na maeneo ambayo yametengwa kwa ajili ya ujenzi wa bomba la mafuta, iwapo mradi huo utaridhiwa kutekelezwa na serikali ya Uganda, ujumbe huo uliruhusiwa
kuondoka.
Hata hivyo, serikali ya Uganda ilieleza kuridhika kwake baada ya kuona hali halisi ya mazingira ya Bandari ya Tanga ikiwa hatua mojawapo ya mchakato wa awali wa ukaguzi kabla ya kupitishwa makubaliano ya ujenzi wa mradi huo. 
Kutokana na hatua hiyo, serikali hiyo inatarajia kutuma timu ya watalaamu kutoka Uganda ili kufanya ukaguzi wa kina kwenye Bandari ya Tanga, kubaini uwapo wa vigezo vinavyotakiwa katika utekelezaji wa mradi.
Akizungumzia hatua hiyo, baada ya kusomewa taarifa ya hali ya Bandari ya Tanga na utendaji wake na kisha kufanya ziara kwenye maeneo mbalimbali, Muloni alisema hali halisi ya mazingira ya bandari hiyo ni ya kuridhisha lakini bado wataalamu kutoka nchini kwake wanalazimika kufanya upembuzi wa kina.
Muloni alimbatana na timu ya wawekezaji wakubwa wa mafuta nchini Uganda kutoka Kampuni za Total, Cnooc na Tulloy.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Tanzania
Justine Ntalikwa, alisema kimsingi Bandari ya Tanga iko katika mazingira mazuri ya kiutendaji kwani inayo eneo zuri la upakiaji na upakuaji wa mizigo na kwamba hakuna msongamano.
Ntalikwa alisema mazungumzo ya mradi huo wa Bomba la mafuta yalianza tangu serikali ya awamu ya nne na kwamba kwa sasa serikali ya Tanzania iko tayari kuupokea mradi na kuutekeleza kwa wakati utakaopangwa.
Awali, Mkurugenzi Mtandaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Dk.James Matarajio, alisema Bandari ya Tanga inakidhi kupokea mradi huo kwa kuzingatia na uwezo wake wa kina irefu cha maji chenye mita 40, hivyo kuweza kupokea mali kubwa za mizigo tofauti na bandari nyingine nchini.
Dk.Matarajio alisema kwa kawaida kina cha kawaida cha maji ni mita 18, hivyo upekee huo wa bandari ya Tanga pamoja na visiwa vinavyozunguka bandari hiyo ambavyo vinatengeneza kingo za asili na kuzuia mawimbi na upepo wa bahari, ni moja ya uwezo uliopo katika kupata mradi wa aina hiyo.
Naye Shigella alisema iwapo mradi huo utaridhiwa kufanyika kwenye bandari ya Tanga, utafungua fursa mbalimbali za kiuchumi, hivyo kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja na mkoa kwa ujumla.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment