Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, March 24, 2016

Waliofariki kwa dalili za ebola wazikwa na Serikali

Wafanyakazi wa ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali wakiwa kwenye gari lililobeba miili ya watu wawili waliofariki dunia kwa maradhi ambayo dalili zake zinafanana na za ugonjwa wa ebola wakielekea katika makaburi ya Mwananyamala, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Florence Majani
By Florence Majani, Mwananchi
Dar es Salaam. Wakati Serikali ikikosa majibu juu ya vifo vya kutatanisha vya watu wawili waliofariki kwa dalili za ebola, miili ya watu hao imezikwa jana na Ofisi ya Mganga Mkuu wa Serikali kwenye makaburi ya Mwananyamala.
Hatia hiyo imechukuliwa ili kuepusha kuenea kwa ugonjwa huo ambao mpaka sasa haujafahamika na sampuli za damu zimepelekwa Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Kenya (KEMR) kwa uchunguzi zaidi.
Jana, ndugu wa marehemu walikusanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) kwa ajili ya mazishi hayo ambayo yalifanywa na Serikali kwa asilimia 100 kwani walitakiwa kukaa mbali bila kusogelea kaburi, kuaga wala kugusa majeneza.
Watu hao walifariki kati ya Machi 16 na 20 katika hospitali hiyo wakipata matibabu baada ya kupata homa kali na kutokwa damu sehemu mbalimbali za miili yao ikiwamo kwenye ngozi.
Mwandishi wetu alishuhudia msafara wa mazishi hayo uliojumuisha basi lililobeba ndugu wa marehemu wote wawili na kutanguliwa na gari maalumu la Serikali lililobeba wataalamu wa afya na gari la tatu lilibeba miili hiyo. Pia, katika gari hilo lenye rangi nyeupe, walikuwamo wataalamu saba wa afya waliokuwa wamevalia mavazi meupe ambayo aghalabu hutumiwa wakati wa kuhudumia wagonjwa wa ebola au homa ya bonde la ufa.
Mmoja wa ndugu wa marehemu, Juma Seromba alisema baada ya Serikali kuamua kuizika miili hiyo, waliamua kuupeleka msiba Iringa.
“Kwa kuwa Serikali imeshaamua hatuna la kufanya, naamini wana nia njema na afya zetu lakini sisi tunachosubiri ni kujua aina ya ugonjwa uliomuua ndugu yetu,” alisema.
Akiwa ndani ya basi tayari kwa kuelekea kwenye mazishi, mmoja wa ndugu wa marehemu kutoka Kilimanjaro, Nicholaus Msuya aliilaumu Serikali kwa uamuzu huo.
“Wametuambia dakika za mwisho kuwa hatutaweza kumzika dada yetu kwa sababu ana dalili za ebola. Tulitaka kuusafirisha mwili lakini daktari kazuia. Hatuna cha kufanya,” alisema.
Mkuu wa Kitengo cha Uchunguzi wa Magonjwa MNH, Dk Praxeda Ogweyo alisema hakuna mgonjwa mwingine aliyefikishwa hospitalini hapo akiwa na dalili hizo.
“Bado idadi ya wagonjwa waliofariki ni walewale wawili hakuna ongezeko, lakini bado tunasubiri majibu ya vipimo kutoka Kenya, ndipo tutajua ni ugonjwa gani,” alisema.
Wiki iliyopita Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu alisema vipimo vya awali vilivyofanyika nchini havijagundua aina ya ugonjwa uliosababisha vifo hivyo.
Ripoti ya hivi karibuni kutoka Shirika la Habari la Uingereza (Reuters) inaonyesha kuwa zaidi ya watu 60 wamefariki dunia Angola kwa dalili kama hizo na baadaye kubainika kuwa ilikuwa ni homa ya manjano (yellow fever). Kadhalika, watu wawili wameripotiwa kufariki dunia huko Kenya kwa homa ya manjano huku mmoja kati yao akibainika kuwa alitokea Angola.

No comments :

Post a Comment