Kwarara Msikitini

airbnb

Dual Citizenship #2

Dual Citizenship #2

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Mwanakwerekwe shops ad

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, March 26, 2016

Yono yafikia wakwepa kodi Zanzibar

Wakati wafanyabiashara waliotuhumiwa kukwepa kodi wakizidi kujisalimisha kulipa madeni yao kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Kampuni ya udalali ya Yono iliyopewa jukumu la kukusanya fedha hizo imeendelea kujitanua na sasa imefungua ofisi visiwani Zanzibar kwa ajili ya kukusanya kodi ya wadaiwa wa Mamlaka hiyo.
 
Akizungumza na Nipashe jana, Mwenyekiti wa Kampuni hiyo, Yono kevela, alisema baadhi ya wafanyabiashara wameshakamilisha fedha walizokuwa wakidaiwa ambapo wamekusanya zaidi ya Sh. milioni 800 na wengine wameahidi kuendelea kulipa taratibu. 
 
Kuhusu Zanzibar, Kevela alisema tayari wamepata cheti kinachowaruhusu kuendesha shughuli zao visiwani humo baada ya kupata kazi ya kukusanya madeni ya Mamlaka hiyo.Alisema wameshaanza maandalizi kwa ajili ya kuanza kazi hiyo rasmi na aliomba ushirikiano kutoka kwa wananchi wa visiwa hivyo.
 
Aidha, alisema wadaiwa wa TRA ambao wamekuwa wakijificha ficha wanapaswa kujisalimisha ili walipe kodi ya serikali kabla ya kampuni hiyo haijawafikia na kuwachukulia hatua za kisheria.
 
Alisema Yono imedhamiria kuwafilisi wadaiwa wa TRA ambao wameshindwa kujisalimisha na ambao wameshindwa kuonyesha ushirikiano wa namna wanavyoweza kulipa deni la serikali.
 
“Iwe ni mifugo, nyumba, kiwanja, sisi tutafilisi mtu ambaye anataka kuleta ujanja ujanja," alisema Kavela na kueleza zaidi, "unajua kuna wafanyabiashara wameonyesha ushirikiano mkubwa na kulipa kodi stahili.
 
"Hivyo hawa wengine tunawasisitiza waige mfano wa hawa wenzao.
 
“Si nia yetu wala serikali kugombana na mfanyabiashara yeyote, sisi tunachotaka ni kodi ya serikali ilipwe.
 
"Sasa mtu asidhani kwamba anaweza kukwepa. Tutamfikia popote pale kuhakikisha serikali inapata stahili yake.”
 
Alisema wafanyabiashara nane kati ya 24 ambao kwa ujumla wanadaiwa Sh. bilioni 18 wameshalipa fedha walizokuwa wakidaiwa kwa Mamlaka.
 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment