dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Saturday, April 2, 2016

CUF yamlaani Balozi wa China

Image result for CUF OF TANZANIA
Siku moja baada ya Balozi wa China, Dk. Lu Youqing, kukaririwa na vyombo vya habari akisema uchaguzi wa marudio Zanzibar uliofanyika Machi 20 ulikuwa huru na haki, Chama Cha Wananchi (CUF) kimelaani kauli hiyo na kusema ni ya kujipendekeza ili kulinda maslahi ya raia wa nchi hiyo walioko nchini.

Juzi Balozi, Dk. Youquing, alikaririwa na vyombo vya habari, akisema kuwa uchaguzi huo ambao CUF iliususia, ulikuwa huru na wa haki.
 
Kufuatia kauli hiyo,  Mkurugenzi wa Mambo ya Nje CUF Taifa, Abdallah Mtolea, katika taarifa yake iliyotumwa kwa vyombo vya habari jana, alieleza:
Serikali inayofahamu maana ya demokrasia, uhuru na haki, haiwezi kusema uchaguzi wa marudio Zanzibar ulikuwa wa huru na haki la sivyo ina matatizo ya kidemokrasia ndani yake.“CUF hatuamini kwamba China haijui demokrasia ikoje," ilisema taarifa hiyo ya Mtolea ambaye ni Mbunge wa Kinondoni, Dar es Salaam.
 
"... wanahalalisha uchaguzi haramu wa marudio Zanzibar kwa sababu ya maslahi yao ya kiuchumi kwa raia wa China nchini Tanzania na huko kwao China, ikizingatiwa kuwa Chama tawala cha China CCP na CCM  wamekuwa na uswahiba wa muda mrefu.”
 
Alisema pia urafiki huo umefanya China kuwa kipofu kuhusu mambo mbalimbali ya ukiukwaji wa haki za binadamu na ukiukwaji wa demokrasia wakihofia kuharibu uswahiba wao na CCM ambao una maslahi zaidi kwa China kuliko Tanzania.
 
“China inaamua kuunga mkono kukandamizwa kwa demokrasia nchini Tanzania ili kujikomba kwa serikali ya CCM waendelee kupata hisani zaidi kwa maslahi ya taifa lao bila kujali CCM kwa kiasi gani inakuwa katili kwa watanzania.” 
Alisema balozi huyo anajipendekeza kwa sababu serikali imekuwa ikiishirikisha China katika tenda mbalimbali, zikiwamo ujenzi wa barabara, madaraja na majengo makubwa nchini.
 
Aliitaka serikali kuwa makini na watu hao ambao hukabiliwa tuhuma za mauji ya tembo za mara kwa mara, likiwamo tukio la Novemba 2013 Mikocheni jijini Dar es Salaam, ambapo wachina watatu wlikamatwa na vipande 700 vya meno ya tembo.
“CUF tunaionya sana China iache siasa kufumbia macho ukiukwaji wa demokrasia nchini kwa maslahi yao na kuitumia Tanzania kujinufasha na rasilimali zilizopo bila kujali amani itakapovunjika hapo baadae. 
 
"Pia tunaitaka serikali kuwa makini na iangalie mahusiano na misaada inayotolewa na China ina malengo gani yaliyofichika kwa taifa letu.” 
China ni nchi ya mfumo wa chama kimoja na katika anga za kimataifa, ina tuhuma nyingi za ukiukaji wa haki za binadamu ikiwemo vifungo vya muda mrefu kwa wapinzani wa serikali yake.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment