dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 1, 2016

Mahakamani kwa kutishia kumuua Rais Dk. Magufuli.


Kondakta Hamimu Seif (42), mkazi wa Mwananyamala Ujiji, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu shitaka kumtishia kumuua kwa maneno Rais Dk. John Magufuli (pichani), kwa kujitoa mhanga.

Mshtakiwa huyo alisomewa shitaka lake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.

Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao, alidai kuwa Machi 10, mwaka huu, katika baa ya Soweto iliyopo Kijitonyama Wilaya ya Kinondoni, mshtakiwa alimtishia kumuua Rais Dk.
Magufuli.

Ilidaiwa kuwa mshtakiwa alitamka: "Kwa haya mambo anayoyafanya Rais Dk. Magufuli, nipo tayari kujilipua kwa kujitoa mhanga ili kumwangamiza," alikaririwa akisema mshtakiwa huyo.

Hata hivyo, mshtakiwa alikana shitaka hilo na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika.

Hakimu Riwa alimtaka mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili watakaosaini hati ya dhamana yenye thamani ya Sh. milioni mbili kila mmoja.

Hata hivyo, mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na kupelekwa mahabusu hadi Aprili 14, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena.

 
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment