dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 1, 2016

Wafanyanyabiashara 5,000 sokoni wajisaidia vichakani


Zaidi ya wafanyabiashara 5,000 wa soko na gulio katika kijiji cha Ntaba Halmashauri ya Busokelo Wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya, wanajisaidia vichakani kutokana na vyoo vya soko hilo kujaa kwa zaidi ya miaka miwili sasa.
 
Aidha, wafanyabiashara hao wameiomba halmashauri hiyo kuwajengea vyoo ili kuondokana na kero hiyo.
 
Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti na gazeti hili, baadhi ya wafanyabiashara hao walisema wamekuwa
wakipata shida kuendesha biashara zao katika mazingira ambayo hayana vyoo.

Walisema baadhi yao hukimbilia nyumba za jirai kujisaidia lakini wengi wao huishia vichakani.Tumbwiza Tweve, mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo, alisema wamekuwa walilipa ushuru kila siku pamoja na siku ya gulio la Jumanne ambalo hukusanya wafanyabiashara kutoka ndani na  nje ya wilaya, lakini halmashauri imekwama kuwajengea vyoo pamoja na kuboresha mazingira.
 
Abraham Alex, mfanyabiashara na mkazi wa eneo hilo, alisema wamechoka kulipishwa fedha wanapokwenda kujisaidia nyumba za jirani na soko hilo.
 
"Tunaiomba serikali itujengee vyoo na kuboresha mazingira hasa maeneo ya choo kilichojaa ili kukwepa magonjwa ya milipuko kikiwamo kipindupindu," alisema Alex.
 
Mfanyabiashara mwingine, Dolnad Bernad, mfanyabiashara alisema halmashauri imeshindwa kuona umuhimu wa kuwajengea vyoo licha ya kukusanya ushuru na kuvuka lengo la mapato kila mwaka.
 
Kwa upande wake, Obadiah Mwakaleko, mfanyabiashara mwingine wa soko hilo, alisema halmashauri
imeweka kipaumbele kutoza ushuru.
 
Ofisa Mtendaji wa kata ya Ntaba, Katamba Reuben, licha ya kukiri kuwapo kwa tatizo hilo, alisema hawawezi kuzungumzia suala hilo kwa madai kuwa masuala ya halmashauri wameagizwa na mabosi wao wasiyazungumze katika vyombo vya habari.
 
Mwenyekiti wa halmashaur hiyo, Anyosisye Njobelo, pia alikiri kuwapo kwa ukosefu huo wa vyoo na kudai kuwa halmashauri tayari imeyatembelea masoko yote yakiwamo magulio ambapo changamoto kubwa waliyoibaini ni ukosefu wa vyoo na wamejipanga kuondoa tatizo hilo.
CHANZO: NIPASHE

No comments :

Post a Comment