dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, April 13, 2016

Makabidhiano ya Ofisi ya Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed (kulia)  akikabidhiana Ofisi na aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini leo katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mjimkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini akitoa shukurani kwa wafanyakazi wa tume ya mipango wakati wa makabidhiano ya Ofisi na  Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed katika ukumbi wa Tume ya Mipango Vuga Mji Mkonge wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
Aliyekuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Dkt.Mwinyihaji Haji Makame Mwadini akiagana na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Khalid Salum Mohammed baada ya makabidhiano ya Ofisi katika viwanja vya Ofisi ya Tume ya Mipango leo Vuga Mji Mkongwe wa Zanzibar baada ya uteuzi uliofanywa na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.
[Picha na Ikulu.]


 
STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar                                 13.4.2016
---
WAZIRI wa Fedha na Mipango Mhe. Khalid Salum Mohammed amesema kuwa Tume ya Mipango ina jukumu kubwa katika kufikia lengo na dhamira ya Serikali katika kipindi hiki cha pili cha Awamu ya Saba katika kuongeza kiwango cha ukusanyaji wa mapato sambamba na ukuaji wa uchumi.

Aliyasema hayo, mara baada ya makabidhiano ya Ofisi ya Tume ya Mipango kati yake na Mhe. Dk. Mwinyihaji Makame Mwadini, hafla iliofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Tume hiyo iliyopo Vuga mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na baadhi ya viongozi na wafanyakazi wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais na Mwenyejiti wa Baraza la Mapinduzi.Waziri Khalid akinukuu hotuba ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Kohamed Shein, aliyoitoa Katika uzinduzi wa Baraza la Tisa la Baraza la Wawakilishi Dk. Khalid alisema kuwa mafanikio katika ukusanyaji wa mapato na kasi ya ukuaji uchumi aliyoeleza Rais itafikiwa kutokana na kujenga mashirikiano ya dhati kwa viongozi na wafanyakazi wote.

“Malengo yote hayo mawili yatafikiwa iwapo kutakuwa na mashirikiano ya kutosha likiwemo lengo la kuhakikisha kuwa kasi ya ukuaji wa uchumi inafikia asilimia 8-10 katika miaka mitano ijayo na lile la kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutoka TZS bilioni 362.8 mwaka 2014/2015 hadi kufikia TZS bilini 800 ifikapo mwaka 2020/2021”,alisema Dk. Khalid.

Katika maelezo yake Dk. Khalid alisisitiza haja ya kufanya kazi kwa kujitolea kwa kila mfanyakazi na katika kila sehemu aliyopo achape kazi kwani hayo ndio matarajio ya Mhe. Rais pamoja na wananchi katika kuiletea Zanzibar maendeleo endelevu.

Waziri Khalid alisema kuwa rasilimali fedha ni muhimu na sekta zote za Serikali zinategemea sana usimamizi na ugawaji wa rasilimali hizo hivyo Tume ya Mipango ina jukumu kubwa katika kusimamia hilo na kuhakikisha linafanikiwa.

Dk. Khalid aliahidi kuimarisha zaidi mashirikiano kati yake, viongozi na watendaji wote wa Tume hiyo ambayo hapo kabla ilikuwa chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora kwa lengo la kufikia matarajio ya wananchi katika kuwaletea maendeleo endelevu.

Aidha Waziri Khalid alimuhakikishia Mhe. Dk. Mwinyihaji kuwa ataendelea kushirikiana nae samba na kuchota hazina ya uzoefu, mawazo, busara na hekima alizonazo katika utendaji wake wa kazi huku akiahidi kuwa hatoacha kujifunza kutoka kwa watendaji na viongozi wa Tume hiyo ya Mipango.

Sambamba na hayo, Dk. Khalid alisisitiza haja kwa viongozi na watendaji wa Tume hiyo kuimarisha zaidi mawasiliano miongoni mwao pamoja na kupeana taarifa zilizosahihi.

Mapema Dk. Mwinyihaji Makame ambaye katika Kipindi cha kwanza katika uongozi wa Awamu ya Saba alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Ikulu na Utawala Bora aliwataka watendaji na viongozi wa Tume hiyo kutoa ushirikiano mkubwa kwa Waziri huyo mpya kama walivyompa yeye katika uongozi wake.

Dk. Mwinyi aliwahakikishia watendaji wa Wizara pamoja na Tume hiyo kuwa wamepata Waziri mchapa kazi na hodari na mwenye kasi katika utendaji wake wa kazi hivyo wakimpa mashirikiano ya kutosha anaamini kuwa mafanikio makubwa yatapatikana katika kuiletea maendeleo Zanzibar.

Dk. Mwinyi alisema kuwa Tume ya Mipango ndio roho ya nchi, kwani ndio inayotoa maelekezo ya matumizi na mipango yote ya kifedha serikalini hivyo kuwepo mashirikiano katika uongozi wa Tume hiyo kutafikia malengo yaliowekwa katika kuiimarisha Zanzibar.

Akitoa neno la shukurani kwa niaba ya watendaji wa Tume ya Mipango, Bi Sharifa Abdalla Khamis aliahidi kuwa wafanakazio wote wa Tume hiyo watampa mashirikiano makubwa Waziri wao huyo mpya huku wakiahidi kuongeza bidii katika utendaji wao wa kazi.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 
 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

No comments :

Post a Comment