Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Wednesday, April 13, 2016

Risasi zarindima ng’ombe wakihakikiwa mahakamani


By Ernest Magashi, Mwananchi 
Bukombe. Milio ya risasi ilirindima jana na kuzua tafrani wakati Mahakama ya Wilaya ya Bukombe ilipohamia mahabusu ya ngo’mbe kuhakiki idadi ya mfugo iliyokamatwa ndani Hifadhi ya Mdendeli Muowisi Kigosi, mkoani Geita.
Inadaiwa kuwa risasi hizo zilizokuwa zikifyatuliwa na watu wasiojulikana zililenga kuwatisha waliokuwa wakiendelea na kazi ya uhakiki iliyokuwa ikisimamiwa na Hakimu Gabriel Kurwijila na kulindwa na askari 35 wa idara ya wanyamapori. Katika tuko hilo, askari 10 walilazimika kujibu mapigo na kufanya eneo hilo kugeuzwa uwanja wa vita.
Baada ya askari wanyamapori na polisi kufanikiwa kuwafurusha wavamizi, waliotokomea porini kabla ya kutiwa mbaroni.
Kazi hiyo iliendelea na kubaini ng’ombe wote 454 wana afya njema ndipo Hakimu Kurwijila alipoahirisha shauri hilo.
Hata hivyo, uhakiki huo ulibaini uwapo wa ng’ombe wa ziada 139 ambao kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mwasimba Hezron, inawezekana waliwafuata wenzao wanaolindwa na askari wa wanyamapori.
Kutokana na hofu ya kuvamiwa wakiwa njiani kurejea Ushirombo, Hakimu Kurwijila aliamuru askari wanyamapori na polisi kuimarisha ulinzi kuhakikisha wote walioko kwenye msafara wanafika salama.
Kesi hiyo inawakabili washtakiwa watano wanaodaiwa kukutwa wakichunga mifungo ndani ya eneo la hifadhi kinyume cha sheria.
Washtakiwa hao leo wanaanza kujitetea na wanatarajiwa kuitwa mashahidi sita kupinga ushahidi wa upande wa mashtaka.
Washtakiwa hao ni Emanuel Wapi, Musa Manyakenda, John Wapi, Nkwabi Ngeleja na Masan Makura.     

No comments :

Post a Comment