dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Friday, April 15, 2016

Ombaomba wabuni mbinu mpya!

…..Zoezi hilo likiendelea.

Kufuatia agizo hilo, gazeti hili juzi lilifanya zoezi la kuzunguka kwenye maeneo yenye ombaombao wengi hasa sehemu za makutano ya barabara kama vile Magomeni Mataa, Fire na Moroco na kubaini kuwa, watu hao wamebadili staili ya kuomba.

Mmoja wa vijana wanaofanya biashara ya kuuza maji katika maeneo ya Fire-Kariakoo jijini Dar alisema:

“Sasa hivi wale wamama na wababa hawaonekani kabisa huku barabarani, wanampiga chenga Makonda. Wanajificha na kuwatuma watoto wao kuja kuomba, halafu mtoto akija kuomba anasema kabisa ametumwa na mama yake ili wapate nauli ya kurudi kwao.“Ndiyo maana huwezi kuwaona wazazi wa watoto wao kule pembeni mwa barabara kama ilivyokuwa awali. Wanakuambia kabisa naomba hela nipate nauli ya kurudi kwetu! Sasa kama una huruma utashindwa kutoa pesa?” alihoji kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Rashidi Omari.




Kwa nini watoto ndiyo wanaonekana?
Inaelezwa kuwa, sababu ya wazazi wa watoto ombaomba kujificha ni kukwepa kukamatwa kwani watoto wao hata wakikamatwa bila wazazi wao ni kazi bure.

“Unajua lengo la serikali ni kuwarudisha ombaomba wote kwao, sasa wakiwakamata watoto tu bila wazazi wao, zoezi haliwezi kufanikiwa, ndiyo maana unatakiwa kupatikana ushirikiano wa kutosha kuwabaini wazazi wa watoto hao wanaowatuma kuomba ili mpango wa kuwarudisha makwao ufanikiwe,” alisema Salim Jumbe, dereva wa daladala inayofanya safari zake kati ya Posta na Makumbusho na kuongeza:

“Halafu hawa watoto hata hawaogopi magari, wanatembea katikati ya barabara bila kohofia pikipiki na magari, ndiyo maana unasikia kila siku wanagongwa lakini hawasikii, waondolewe kwa nguvu tu.”
Ni tatizo kubwa


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda.

Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kuwa ombaomba hao ni tatizo kubwa jijini Dar kwani wamekuwa wakisababisha usumbufu mkubwa kwa wasafiri na hata watembea kwa miguu.

“Yaani kazi hii imeonekana kama ni halali sasa, kila kukicha wanazidi kuongezeka na wengine usipowapa pesa wanakutukana, kukukwangulia gari yako na hata kukutemea mate. Mbaya zaidi ukitoa pesa yako kwa kumuonea huruma, kesho lazima aje tena barabarani, matokeo yake wananogewa.

“Mimi nadhani hili aliloanzisha Makonda liungwe mkono na watu wote, kweli wana hali mbaya lakini naamini kuna maisha mengine wanaweza kuishi kuliko haya ya kuja kuombaomba,” anaeleza mama Janeth wa Kinondoni.

No comments :

Post a Comment