dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Thursday, April 14, 2016

Tanzania kuendelea kunufaika na miradi ya Marekani

Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga
By Vicky Kimaro na Suzan Shao, Mwananchi
Dar es Salaam.  Wakati misaada ya Bodi ya Shirika la Changamoto za Milenia (MCC), ikisitishwa, Marekani imeihakikishia Tanzania bado itaendelea kupata Dola 700 milioni ambazo ni sawa na Sh152 trilioni  katika kufadhili miradi ya afya na elimu.
Katika Kikao cha  Waziri wa Mambo ya Nje,Afrika Mashariki,Kikanda na Ushirikiano wa Kimataifa Dr Augustine Mahiga na Balozi wa Marekani nchini Mark Childress  kilichofanyika juzi, lengo lilikuwa ni Tanzania kutaka kuhakikishiwa iwapo miradi inayofadhiliwa na Marekani nchini kama bado nchi hiyo itaendelea kuifadhili ama  itasitishwa.
Hata hivyo, Balozi huyo wa Mareani nchini alimuhakikishia Waziri Mahiga kuwa licha ya changamoto  mbali mbali za kisiasa zilizopo nchini, bado nchi yake imeona umuhimu wa  kuendeleza  mahusiano katika kutoa misaada ya maendeleoa hasa katika sekta ya elimu na afya

No comments :

Post a Comment