dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Tuesday, April 12, 2016

Waziri Hamadi Rashid aanza kazi kwa kasi ya Magufuli


Siku moja tu baada ya kuapishwa kuwa waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Zanzibar Mhe Hamad Rashid ameanza kazi kwa kishindo kwa kupiga marufuku harakati za siasa wizarani na kuahidi hatosita kumwajibisha mfanyakazi atakayeshindwa kutekeleza jukumu lake.

Mhe Hamad Rashid ambaye ni waziri kutoka chama cha upinzani ndani ya seriklai ya CCM Zanzibar ametoa tahadhari hiyo huko Bungi mkoa wa kusini Unguja aliposhiriki zoezi la upandaji miti la Zanzibar ambalo linaendelea sehemu mbalimbali Unguja na Pemba huku ikiwa ni siku yake ya kwanza kuanza kazi ambapo amesema sasa ni wakati wa kazi na sio siasa anayetaka kujishugulisha na siasa aiache wizara huku akisisitiza amepania kuona sekta hizo zake zinaleta mafanikio na mabadiliko.Mhe Hamad Rashid amewataka wafanyaakzi wa wizara hiyo kuelewa umuhimu wa wizara yao ambayo inachangia asilimia 75 ya ajira na asilimia 30 ya pato la serikali huku akiahidi kuwa mkweli na mchapa kazi lakini hatokuwa na huruma kwa mfanyakazi ambaye haelewi jukumu lake la kuwepo kazini, huku katibu mkuu wa wizara hiyo Affan Maalim amesema zoezi hilo limekuwa la mafanikio makubwa ambapo linaendelea Unguja na Pemba.

Katika harakati hizo ITV ilifanikiwa kushinda na kupewa nafasi ya kupanda miti wa Mdimu ambao ulipewa jina la ITV kutokana na chombo hicho kuwa mstari wa mbele katika habari na kuhifadhi mazingira.

No comments :

Post a Comment