dual citizenship

Pemba Paradise

Zanzibar Diaspora

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

ZNK Patreon

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Wednesday, August 24, 2016

Dk Shein Afungua Mkutano wa Kongamano la Tatu la Watanzania Wanaoishi Nje ya Nchi Diaspora!


 
















STATE HOUSE ZANZIBAR
OFFICE OF THE PRESS SECRETARY
PRESS RELEASE
Zanzibar 24.08.2016
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar zimekuwa zikipanga na kutekeelza mikakati mbali mbali ya kukuza uwekezaji kwa kuweka mazingira mazuri yanayowavutia na kuwashajiisha wawekezaji wa ndani na nje ya nchi wakiwemo ‘Diaspora”.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo katika hotuba yake ya ufunguzi wa Kongamano la tatu la Diaspora lililofanyika huko katika ukumbi wa hoteli ya Zanzibar Beach Resort, Mbweni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.

Katika hotuba yake hiyo, Dk. Shein alisema kuwa Serikali zote mbili zimepanua fursa za uwekezaji katika sekta ya utalii, biashara, viwanda, kilimo, ufugaji, uvuvi wa bahari kuu, ujenzi wa nyumba, na sekta nyengine mpya zinazoibuka katika uchumi wa nchi ikiwemo sekta ya mpya ya gesi na mafuta ambayo kwa Zanzibar inatarajiwa kuimarika katika miaka michache ijayo.

Dk. Shein aliwataka Wana “Diaspora” kuendelea kuwa na ujasiri na wawe tayari kuzichangamkia fursa hizo kama wanavyofanya wana “Diaspora” wa baadhi ya nchi ambazo wameweza kuleta mabadiliko makubwa katika nchi zao ikiwemo Ghana, Brazil, Ethiopia na India.

Katika utekelezaji wa dhamira ya kuunganisha utalii na uwekezaji, Serikali zote mbili zimekuwa zikipanga mikakati imara ya kuendeleza miundombinu kwa kuzingatia ukweli kuwa miundombinu ndiyo daraja bora la kuziunganisha sekta zote za kiuchumi ikiwemo sekta muhimu ya utalii.

“Nakushaurini mzitumie fursa zilizopo za kitaalamu katika sekta mbali mbali, nchi yetu inahitaji wataalamu katika nyanja nyingi hasa katika maeneo mapya ya kiuchumi yanayoibuka na yale yaliopewa kipaumbele na Serikali zetu hivi sasa”,alisema Dk. Shein.

Aidha, Dk. Shein alisema kuwa kwa upande wa Zanzibar, Serikali imo katika hatua za mwisho za kutayarisha Sera ya “Diaspora” ambayo itapitishwa wakati wowote kuanzia hivi sasa ambapo baada ya kukamilika itafafanua na kuweka wazi dira na dhamira za Serikali katika utekelezaji wa masuala muhimu yanayohusiana na Diaspora.

Alieleza kuwa Sera hiyo itaelekeza njia bora za kutuma na kupokea fedha pamoja na kuimarisha misaada ambayo wamekuwa wakiitoa kwa ajili ya utekelezaji wa mipango ya maendeleo sambamba na kubainisha sheria na wahusika muhimu katika kuyashughulikia masuala ya “Diaspora”.

Pamoja na hayo, Dk. Shein aliwanasihi Wana “Diaspora” waendelee kuwa mabalozi wazuri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika nchi wanazoishi pamoja na kuwa mfano wa tabia njema ili waendeleze sifa ya ukaribu, urafiki na usalama ambayo Tanzania na raia wake wamejijengea na kutambulika katika mataifa yote duniani.

“Zielezeeni sifa nzuri za nchi yetu pamoja na watu wake”,alisema Dk. Shein na kuwataka Wana ‘Diaspora” kuendelea kuishi kwa kuzingatia misingi ya urafiki na udugu huku mkiwa na mapenzi makubwa baina yao pamoja na nchi yao ya asili.

Sambamba na hayo, Dk. Shein aliwataka wana ‘Diaspora’ kuendeleza utamaduni wa kuja kutembea nyumbani kila baada ya muda, jambo ambalo ni muhimu na linaimarisha mapenzi baina yao na ndugu, jamaa na wazazi wao.

Dk. Shein pia, alitumia fursa hiyo kuwataka Wana “Diaspora” wakija nyumbani kufanya jitihada za kuja na watoto wao ili nao wapate fursa za kuyaona mambo mbali mbali ili waweze kuyathamini mambo ya nchi yao ya asili.

“Jengeni utamaduni wa kuja nyumbani mara kwa mara kwa ajili ya kufuatilia mambo yenu na fursa zilizopo, msipende kuagiza, zingatieni ule usemi maarufu wa lugha yetu kuwa “kuagiza kufyekeza”, aliongeza Dk. Shein.

Dk. Shein alitoa shukurani kwa uongozi wa Ofisi ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pamoja na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa kuandaa Kongamano hilo.

Mapema wakitoa neno la utangulizi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Dk. Augustine Mahiga na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Issa Haji Gavu kwa nyakati tofauti walieleza kuwa Kongamano hilo ni la tatu kufanyika ambalo la kwanza lilifanyika mwaka 2014 na la pili 2015 yote yalifanyika Dar-es-Salaam.

Viongozi hao walitoa shukurani kwa Taasisi za Umma na Taasisi binafsi pamoja na mashirika mbali mbali ya serikali na yasiokuwa na serikali yaliosaidia kuchangia Kongamano hilo pamoja na kulidhamini.

Waziri Mahiga alieleza kuwa Kongamano hilo limelenga katika kuwahamasisha na kuwashajiisha Wana “Diaspora’ kushiriki katika kuendeleza sekta ya Utalii nchini ikiwa ni njia mojawapo ya kukuza uwekezaji hapa Tanzania.

Aidha, alieleza kuwa kauli mbiu ya Kongamano hilo imeamuliwa kuwa ni “Bridging Tanzania Tourism and Investment: A new Outlook”, yaani Kuiunganisha Sekta ya Utalii na ya Uwekezaji: Mtazamo Mpya.

Nao Wana “Diapora” walitoa pongezi zao kwa Serikali zote mbili na kueleza kufarajika kwao na juhudi za Serikali hizo katika kuwashirikisha katika kupanga mipango ya maendeleo yao ya nchi yao.

No comments :

Post a Comment