Top Leaderboard Advert

Mwanakwerekwe shops ad

ZanzibarNiKwetuStoreBanner

Zanzibar Diaspora

High class shops @ Fuoni

High class shops @ Fuoni

Scrolling news

************ KARIBUNI..................Contact us for any breaking news or for any information at: znzkwetu@gmail.com. You can also fax us at: 1.801.289.7713......................KARIBUNI

Adsense Marquee

Thursday, August 11, 2016

Shehia ya Shauri Moyo Kupita Nyumba Hadi Nyumba

Na Miza Kona/ Rahma Khamis Maelezo – Zanzibar.
Baraza la Manispaa Zanzibar kwa kushirikiana na shehia ya Shaurimoyo watafanya ukaguzi Nyumba hadi nyumba katika Shehia hiyo kuangalia Karo kwa lengo la kukabiliana na maradhi ya mripuko yanayoweza kujitokeza.

Hatua hiyo inakuja baada ya Wananchi hao kukaidi maagizo ya Shehia hiyo na hivyo Sheha huyo kuamua kuchukua umamuzi wa kulishirikisha Baraza la Manispaa ili kuwadhibiti wananchi wenye tabia ya uchafu katika Shehia hiyo.

Sheha wa Shehia ya Shaurimoyo Mohamed Mohamed Salum ameyasema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa habari kuhusiana na mikakati mbalimbali ya kuimarisha usafi katika Shehia yake.

Amesema tabia ya uchafu kwa Wananchi wengi wa Shehia hiyo imejengeka bila kukubali mabadiliko jambo ambalo limemfanya Sheha huyo kushirikiana na Baraza la Manispaa kuchukua hatua kali za kisheria kukabiliana na Watu hao.Sheha Mohamed ameongeza kuwa baadhi ya Wananchi wamejijengea tabia kutupa taka ovyo katika Mtaro wa maji machafu na hivyo kuleta uharibifu wa mazingira.

Aidha Sheha huyo ameeleza kuwa kumejitokeza mtindo kwa baadhi ya wananchi kujenga kuta katika chochoro bila ya idhini ya serikali hivyo hupelekea kuziba njia na kuleta usumbufu pindi majanga ya moto yanapotokea.

“Watu wanajenga kuta katika chochoro kwa nguvu zao bila ya idhini ya serikali na kusababisha usumbufu wakati wa maafa ya moto au mgojwa njia washaziziba, hatukubali na hatutomvumilia mtu, hatua kali za kisheria tutazichukua kwa yoyote atakaefanya hivyo,”amesisitiza Sheha huyo.

Amefahamisha kuwa Shehia imeweka utaratibu maalum wa kukusanya taka na kuzitupa sehemu husika ambapo Mwananchi hutakiwa kulipia Sh.200 na kwayule atakayeshindwa hukopeshwa hadi mwisho wa mwezi.

Hata hivyo sheha Mohamed amewaomba watu wenye uwezo kuwapatia vifaa vya kufanyia usafi ikiwemo bero, viatu, mapauro na glavu kwa ajili ya kujikinga na uchafu ili waweze kudumisha usafi katika shehia yao.

Aidha amewataka wananchi kuwa na ushirikiano wa pamoja na kufuata masharti ya serikali na watu wa Afya kwa kufanya usafi kwani kufanya hivyo kutaepukana na maradhi ya mripuko na kipindupindu.


MWISHO
IMETOLEWA NA IDARA YA HABARI MAELEZO ZANZIBAR

No comments :

Post a Comment